HABARI MPYA LEO  

Utajiri wa Kanumba, kamati kuisaidia familia.

By Maganga Media - Apr 15, 2012

UTAJIRI wa aliyekuwa msanii maarufu katika tasnia ya filamu nchini, marehemu Steven Kanumba, mpaka sasa umeendelea kuwa siri baada ya familia yake kusita kuuzungumzia kwa maelezo kwamba ni mapema mno na bado wanamlilia mtoto wao.

Mdogo wa marehemu Kanumba, aliyekuwa akiishi naye Sinza Vatican, Dar es Salaam mpaka hadi mauti yalipomfika, Seth akizungumza na Mwananchi Jumapili nyumbani hapo juzi, alisema; “Mama hayuko tayari kuzungumzia masuala ya mali, ni mapema mno bado anamlilia mtoto wake.”

Seth alisema siyo rahisi katika muda mfupi kama huu kufahamu mali za marehemu, lakini familia ikitulia na kutekeleza jukumu hilo kwa ukamilifu, taarifa zitatolewa kwa jamii kama  itaonekana kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Naye Gabriel Mtitu anayetajwa na wachungaji wa Kanisa la AIC, alilokuwa akisali Kanumba enzi za uhai wake, kuwa ndiye aliyemuingiza kwenye uigizaji, alisema imeundwa Kamati kumsaidia mama mzazi wa marehemu kufuatilia na kuweka salama mali zote alizokuwa akimiliki.

“Kamati itamsaidia mama kufuatilia mali za marehemu ikiwemo mikataba ya kazi aliyoiingia ndani na nje ya nchi, mashamba, nyumba, uendelezaji wa kampuni yake,” alibainisha Mtitu.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII