HABARI MPYA LEO  

Mbunge aanguka viwanja vya bunge

By Maganga Media - Apr 15, 2012


Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Clara Mwituka, ameanguka katika viwanja vya Bunge mjini hapa na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu. Tukio hilo lilitokea jana asubuhi, wakati mbunge huyo alipofika kwa ajili ya semina ya wabunge wote iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

Inadaiwa mbunge huyo alianza kujisikia vibaya akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jambo lililomfanya kutoka nje ya ukumbi huo. Hata hivyo, akiwa katika viwanja vya Bunge, alianguka na kuwafanya wataalam wa afya waliokuwa katika zahanati ya Bunge kuitwa kwa ajili ya kumpatia huduma.

NIPASHE Jumapili ilishuhudia mbunge huyo akiwa amebebwa kwenye baiskeli ya miguu mitatu (wheel chair), akitolewa katika viwanja hivyo huku akisaidiwa na wataalamu wa afya na Mbunge (CCM), Murtaza Mangungu, kupelekwa katika zahanati ya Bunge.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Zainabu Chaula, alithibitisha kupokelewa kwa mbunge huyo na kwamba amelazwa katika wodi za grade one. Alisema bila kufafanua, Dk Chaula alisema baada ya vipimo ilithibitika kuwa alikuwa na homa.

“Hakuanguka bali alikosa nguvu na kwenda mwenyewe katika zahanati ya Bunge ambapo aliletwa hapa kwa ajili ya matibabu. Hajambo anaendelea vizuri,”alisema.

GAZETI LA NIPASHE
 

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII