HABARI MPYA LEO  

Uchaguzi nchini Ufaransa kampeni zahitimishwa

By Maganga Media - Apr 20, 2012


Wagombea urais nchini Ufaransa, Francois Hollande (kushoto) na Nicolas Sarkozy (kulia)
Wagombea urais nchini Ufaransa, Francois Hollande (kushoto) na Nicolas Sarkozy (kulia)

Mamlaka nchini Ufaransa zimetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yoyote ambaye atachapisha matokeo ya uchaguzi kabla ya kupigwa kwa kura zikiwa zimesalia siku mbili kbala ya wananchi wa taifa hilo hawajashiriki duru la kwanza la kinyang'anyiro cha uchaguzi.
 

Wananchi wengi wa Ufaransa hawajui watamchagua nani kwenye uchaguzi wa hapo jumapili huku upinzani mkali ukionekana kati ya Rais Nicolas Sarkozy anayetetea wadhifa wake na Mpinzani wake Francois Hollande. Onyo hilo linatolewa wakati ambapo hii leo wagombea wa kiti cha urais nchini humo wanatarajiwa kuhitimisha kampeni zao ikiwa imebaki siku moja kabla ya wananchi kuanza kupiga kura kuchagua rais mpya.

Rais wa zamani wa Ufaransa Jacque Chirac ametangaza wazi kumuunga mkono kiongozi mkuu wa upinzani Francois Holande hatua inayoelezwa kuchochewa kisiasa zaidi na uhasama uliopo kati yake na rais Sarkozy.

Chirac mwenye ushawishi mkubwa kwenye siasa za Ufaransa ametangaza azma yake hiyo ikiwa imebaki siku moja kufikia tarehe rasmi ya uchaguzi mkuu, uamuzi ambao unaelezwa utakuwa pigo kwa kambi ya rais Sarkozy.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema licha ya kwamba huenda rais Sarkozy akatetea nafasi yake lakini haitakuwa rahisi kama uchaguzi uliopita kwakuwa safari hii mpinzani wake anaungwa mkono sana.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII