HABARI MPYA LEO  

Yanga kumaliza hasira kwa Simba.

By Maganga Media - Apr 20, 2012

BEKI wa Yanga, Nadir Haroub amesema pamoja na kupoteza ubingwa sasa wanachongalia ni kulinda heshima ya timu yao kwa kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa mwisho Ligi Kuu dhidi ya mahasimu wao Simba.

Akizungumza na Mwananchi toka mjini Kagera, Nadir alisema ushindi watakaoupata katika mechi hiyo ndiyo pekee utakaowafuta machungu ya kushindwa kutetea ubingwa wao. "Nitafurahi sana endapo Simba watachukua ubingwa huo na siyo Azam," alisema Nadir.

Naye Katibu mkuu wa Yanga, Selestin Mwesigwa alisema  kushindwa kutetea taji msimu huu, haina maana kwamba  timu yao siyo bora. Mwesigwa alisema mwisho wa msimu watakutana kwenye Kamati za timu hiyo kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosa ubingwa dakika za mwisho.

"Klabu ina mipango ya muda mfupi na muda mrefu hivyo mwisho wa msimu miongoni mwa mipango ya muda mrefu tutakayojadili ni kwa nini tumeukosa ubingwa," alisema Mwesigwa.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII