HABARI MPYA LEO  

Salva Kiir asitisha mapigano

By Maganga Media - Apr 20, 2012

Wanajeshi wa Sudan Kusini
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir ameamrisha wanajeshi wake kuondoka kwenye visima vya Heglig katika mpaka unaozozaniwa kati yake na Jamuhuri ya Sudan. Wanajeshi wa Sudan Kusini waliteka eneo la Heglig wiki jana ambapo walilaumu utawala wa Khartoum kutumia mahala hapo kama ngome ya kufanya mashambulio.
Hapo Alhamisi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon alitaja kuwepo kwa wanajeshi wa Sudan Kusin kama kinyume na sheria ya kimataifa.
Hata hivyo Umoja wa Mataifa ulitaka Jamuhuri ya Sudan kusimamisha mashambulio dhidi ya Sudan Kusini .

Makabiliano kati ya pande zote yalitishia kuzuka kwa vita vingine. Sudan Kusini ilijiondoa kwa Jamuhuri ya Sudan mwaka jana kufuatia muafaka wa amani ulioafikiwa mwaka 2005 baada ya vita vya zaidi ya miongo miwili.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII