HABARI MPYA LEO  

Mourinho aitakia Chelsea ushindi

By Maganga Media - Apr 26, 2012


Jose Mourinho
Meneja wa zamani wa Chelsea anasema angelipenda kuona Chelsea wakiibuka washindi katika fainali dhidi ya Bayern Munich. Jose Mourinho, meneja wa Real Madrid ya Uhispania, amesema angelipenda Chelsea ya Uingereza ipate ushindi itakapocheza na Bayern Munich katika mechi ya fainali ya soka ya klabu bingwa mjini Munich.

Mourinho amesema hayo baada ya Real kushindwa na timu ya Bayern Munich ya Ujerumani kupitia mikwaju ya penalti.

Chelsea walifuzu kuingia fainali baada ya kuishinda Barcelona, pia ya Uhispania, na kwa muda mrefu wakicheza wakiwa 10. "Bila shaka ningelipenda Chelsea wawe washindi. Walikuwa ni mashujaa kuishinda Barcelona wakiwa na wanaume kumi uwanjani," alisema meneja huyo wa zamani wa The Blues.

"Mimi ninajivunia wachezaji wangu, lakini katika mechi kubwa kama hiyo, tulihitaji nguvu zaidi na tulipaswa kuwa wachangamfu."

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII