Kili yaibua vipaji Dodoma
By Maganga Media - Apr 29, 2012
BAADA ya siku mbili za usaili wa jumla ya washiriki 247 waliowania nafasi ya kupanda jukwaa moja na washindi wa Tuzo za Kili wa mwaka 2012, hatimaye wawakilishi wa Mkoa wa Dodoma wamepatikana jana mchana katika zoezi lililoonekana kuwa gumu kutokana na washiriki hao kuwa na vipaji vya hali ya juu vinavyofanana. Katika zoezi hilo lililofanyika katika ukumbi wa Club maarufu mkoani humo inayojulikana kwa jina la 84, kati ya wasanii 247, ni watano tu wenye jinsia ya kike ndio walijitokeza kushiriki. Kazi ya mchujo kwa wasanii hawa ilifanyika kwa takriban saa 29 ambapo majaji wanne waliifanya, wakiongozwa na msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule, na mwanamuziki mwingine maarufu wa muziki huo Juma Kassim Nature, mshindi wa Tuzo ya Wimbo Bora wa Ragga kwa msimu huu Queen Darleen na Mhariri wa Burudani wa Magazeti ya Mwananchi Communications. Katika mchujo wa kwanza, jumla ya wasanii 200 waliondolewa katika mashindano, kisha wakabakia 47 ambao nao walipopita mbele ya majaji kwa mara ya pili, walijikuta wakiondoka 27 na kubakia 20 ambao waliingia katika fainali ya awali iliyofanyika siku iliyofuata. |
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII