HATMA YA LISSU LEO
By Maganga Media - Apr 27, 2012
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma imepanga leo kuwa siku ya kutoa hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya ubunge jimbo la Singida Mashariki, yaliyompa ushindi mbunge wa sasa, Tundu Lissu.
Kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na Jaji Moses Mzuna kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro, imepangwa kutolewa hukumu leo ambapo maelfu ya wakazi wa mkoa huo na maeneo jirani watahudhuria.
Makada wawili wa CCM walifungua kesi hiyo dhidi ya Lissu wakipinga ushindi wake kwa kile walichodai kuwa katika uchaguzi huo wa mwaka 2010, mgombea huyo wa Chadema alishinda kwa mizengwe.
Walalamikaji katika kesi hiyo ni Shabani Selema na Pascal Itadu ambao wanaiomba mahakama hiyo kutengua matokeo hayo kwa madai kuwa baadhi ya taratibu, kanuni na sheria, zilikiukwa.
Katika kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa tangu Machi 12 mwaka jana, Lissu alikuwa mshtakiwa wa kwanza. Washtakiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa uchaguzi huo jimbo la Singida Mashariki.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII