Mwanajeshi 'muuaji ' ahamishiwa Kuwait
By Maganga Media - Mar 15, 2012
Maafisa wa jeshi la Marekani wamebainisha kuwa askari wa jeshi hilo ambaye anatuhumiwa kuwaua raia kumi na sita wa Afghanistan mwishoni mwa wiki, ameondolewa nchini humo.
Mwanajeshi huyo huenda akahukumiwa kifo |
Waathirika wa shambulio hilo tisa kati yao wakiwa ni watoto, waliuawa kwa kupigwa risasi majumbani mwao, usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita.
Kuondolewa kwa mwanajeshi huyo huenda kukachochea hasira kali nchini Afghanistan hasaa baada wabunge nchini humo kutaka afunguliwe mashataka nchini mwao.
Lakini ilikuwa wazi hilo halingetendeka. Kulingana na sera za Marekani mwanajeshi wawake wowote anayepatikana na hatia sharti afunguliwe mashataka kulingana na sheria za jeshi lake. Hata hivyo mwanajeshi huyo bado hajafunguliwa mashataka na kwa hivyo kufikia sasa bado hajajulikana. Kulingana na maafisa ikiwa atakuwa anahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kubainisha ikiwa ana akili timamu, basi itachukuwa muda kabla ajulikane au hata kufunguliwa mashataka.
Waziri wa ulinzi Leon Panetta amesema ikiwa atapatikana na hatia huenda akahukumiwa kifo. Na kufuatia visa vya hivi karibuni vya wanajeshi hao ambavyo vimechochea uhusiano mbaya kati Marekani na raia wa Afghanistan, kumekuwa na tetesi kuwa Rais Obama huenda aka harakisha mpango wa kuondoa vikosi hivyo nchini humo. Lakini akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ambaye, Rais Obama amesema watafuata ratiba ile ilioko.
Viongozi hao wawili wamesema wanajeshi wao wataondoka Afghanistan baada ya kuwaandaa wanajeshi wa nchi hiyo vizuri kusimamia usalama wao. Wameongeza kuwa malengo yao yanatimia kwa kuwa kufikia sasa karibu nusu ya nchini hiyo sasa inadhibitiwa na wanajeshi wa Afghanistan. Vikosi vya Marekani na Uingereza vinatarajiwa kuondoka Afghanistan ifikiapo mwaka 2014
http://maganga-resources.blogspot.com
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII