HABARI MPYA LEO  

Eritrea:‘Hatujibu mashambulizi ya' Ethiopia

By Maganga Media - Mar 18, 2012

Wananchi wa Eritrea
Eritrea imesema haitaingia kwenye ‘mtego wa kujibu mapigo’ baada ya Ethiopia kufanya shambulio mpakani katika kambi zake tatu za kijeshi.
"Ni wale wasiojua gharama ya vita ndio wenye njaa ya kujitosa vitani," Waziri wa Habari wa Eritrea aliliambia Shirika la Habari la AFP.

Ethiopia ilisema ilishambulia kambi hizo tatu za jeshi kwa kuwa zinatoa mafunzo kwa makundi ya waasi. Nchi hizo mbili zilipigana kwa ajili ya mpaka kuanzia mwaka 1998 mpaka 2000.
Marekani imetoa wito kwa nchi zote mbili ‘kujizuia na kuepuka hatua nyingine yoyote ya kijeshi.’ Shambulio hilo limezusha wasiwasi kuwa mahasimu hao wangeweza kurejea kwenye uhasama kamili lakini Eritrea imeondoa hisia za wasiwasi huo.


"Tulipigana vya kutosha kwa miaka 30 na hatutavutwa tena kuingia vitani katika uchokozi usiokubalika kama huu." Bw Ali aliiambia AFP. "Raia na serikali ya Eritrea haiwezi kuendekeza na haitaingia kwenye mtego wa kijanja kama huo," taarifa ya Waziri wa Habari ilisema. Ilisema shambulio hilo lilimaanisha kupoteza lengo kwani ‘Ethiopia inaikalia kinyume cha sheria ‘ katika milki ya Eritrea pamoja na matatizo yake ya ndani.

Eritrea inaituhumu Ethiopia kwa kukataa kuondoka kwenye vijiji vya Badme, ambako vita vya mpaka vilianzia licha ya Tume ya mipaka yaThe Hague ya mwaka 2002 kuamua kuwa ulikuwa wa Eritrea. Watu kadhaa waliuawa na wengine kukatwa wakati shambulio la kambi hizo tatu lilipofanywa kiasi cha kilometa 18 (maili 11) ndani ya Eritrea na msemaji wa Ulinzi wa Ethiopia alisema, hakujawa na habari zaidi.

http://maganga-resources.blogspot.com

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII