Wataalamu wa Utawala Bora kutua nchini Mei
By Maganga Media - Feb 24, 2012
|
JOPO la watalaamu wa masuala ya Utawala bora linatarajiwa kuwasili nchini kuanzia Machi 2 mwaka huu, ili kutathimini hali ya Utawala Bora na Mpangokazi wa Serikali ya Tanzania na kuanisha changamoto zake.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu Mtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora Tanzania (APRM) Rehema Twalib ilisema watalaamu hao wataingia nchini ili kukutana na makundi mbalimbali.
Twalib alisema watalaamu hao wataainisha namna nchi ya Tanzania inavyoshughulikia changamoto za kiutawala bora zinazoikumba nchi.Alisema watalaamu hao watatua nchini kwa takribani wiki tatu kuanzia Machi 2 ili kukutana na wadau mbalimbali wa masuala ya utawala bora.
Makundi hayo yatakayokutana na wataalamu wa masuala ya utawala bora (CRM) kutoka makao makuu ya APRM ni pamoja na viongozi wa Serikali, wabunge, wawakilishi wa vyama vya kiraia, vyombo vya habari na wasomi wa vyuo vikuu.
Pia jopo hilo litakutana na vyama vya wafanyakazi, asasi za kijamii zilizoko vijijini na wabia wa maendeleo walioko nchini ili kutoa ripoti ya Thatmini ya utawala bora.
Alisema jopo hilo linajumuisha wataalamu wa fani mbalimbali katika nchi za Afrika ambalo litafanya kazi ya kukutana na kila kundi ili kuweza kupata matatizo ili kuweza kuitathimini Tanzania.
"Mikutano ya wataalamu hawa itakuwa na lengo la kushauriana juu ya changamoto za utawala bora na kutoa mapendekezo juu ya hatua muhimu zinazopaswa kuchukuliwa," alisema.
Alisema nchi 33 kati ya nchi 54 za Afrika ndizo zilizosaini kuingia katika mchakato wa kujitathimini katika utawala bora ambapo Tanzania ilijiunga mwaka 2005.Aliaisema Tanzania imekamilisha mchakato wa kujitathmini wa ndani ya nchi toka mwaka 2009 na kwamba ripoti ya Ndani ya Nchi na Mpangokazi vilihuishwa mwaka jana.
Twalib alisema watalaamu hao wakiwa hapa nchini watafanya kazi ya kuhakiki repoti na kutoa hali halisi ya utawara bora utakaoainisha Tanzania inavyopaswa kufanya.
Alisema mchakato huo wa APRM hufanyika kila baada ya miaka minne ili kuzipa nchi za afrika kutatua kero.
Twalib alisema hatua hiyo ya wataalamu kuingia nchini imekuja baada Serikali ya Tanzania kuwaalika kuja kufanya thatimini. |
http://maganga-resources.blogspot.com
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII