HABARI MPYA LEO  

Msajiri wa Vyama Vya Siasa nchini, John Tendwa


MSAJILI wa Vyama Vya Siasa nchini, John Tendwa ameelezea kukerwa na malumbano ya Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Mbunge wa Musoma mjini (Chadema), Vincent Nyerere na kuonya kuwa kauli zao ni hatari na zinajenga chuki ndani ya taifa.


Malumbano kati ya wanasiasa hao, yaliibuka baada ya Mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM kudai kuwa kwa kipindi chote alichowahi kufanyakazi na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hakuwahi kusikia kama kulikuwa na mwanafamilia anayeitwa Vincent Nyerere.


Juzi, malumbano hayo yalichukua sura mpya  baada mtoto wa kiume wa Mwalimu Nyerere, Madaraka kuibuka na  kuthibitisha kuwa Vincent ni mdogo wao na ni mwanafamilia ya Mwalimu, kwani ni mtoto wa baba yao mdogo, marehemu Josephat Kiboko Nyerere.


Hata hivyo, Madaraka katika majibu yake mafupi kwa Mwananchi aliyoyatuma kwa barua pepe, aliweka wazi kwamba asingependa kujibu maswali mengine zaidi ya kuthibitisha undugu wake na Vincent, akihofu kuingilia kampeni za uchaguzi mdogo wa Arumeru na kushauri maswali mengine yajibiwe na Mkapa mwenyewe au mbunge huyo.  


Tendwa alisema kauli ya Mkapa dhidi ya Vincent na majibu ya mbunge huyo, ni kinyume cha siasa zilizotarajiwa katika uchaguzi huo mdogo ukizingatia kwamba kauli hizo zinakuja katika kipindi cha kampeni, jambo ambalo linaweza kuibua chuki katika taifa na kusababisha vurugu ndani ya jamii.


CHANZO: Gazeti la Mwananchi. SOMA ZAIDI
Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) imetangaza maelekezo muhimu kwa waombaji wa vyuo vikuu waliochaguliwa mwaka jana lakini hawakuweza kuripoti vyuoni kwa sababu mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa hii, waombaji wote waliochaguliwa mwaka jana na hawakuripoti vyuoni HAWATARUHUSIWA KUOMBA TENA MWAKA HUU mpaka waandike barua TCU kabla ya Tar 30.03.2012 kuelezea:

1. Jina la chuo na kozi uliyokuwa umechaguliwa
2. Sababu za kushindwa kuripoti
3. Namba ya mtihani wa kidato cha nne na cha sita pamoja na miaka ya kumaliza
4. Maandalizi yako ya kukabiliana na changamoto zilizokufanya ushindwe kuripoti chuo mwaka wa masomo uliopita
IMETOLEWA NA KATIBU MKUU TCU






All letters should be submitted to TCU before 30th March 2012 and be addressed to:
Executive Secretary
Tanzania Commission for Universities
P. O. Box 6562
DAR ES SALAAM.
For more information contact TCU through:
Tel No.: (255) (22) 2772657
Fax:  (255) (22) 2772891
Website: www.tcu.go.tz

Issued by
TCU Executive Secretary


Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amerejea nchini kutoka Ujerumani alikokwenda kwa matibabu na kuzungumzia afya yake akisema anasumbuliwa na ugonjwa wa macho,na kujitutumua kwa kukunja ngumi huku akitamba kuwa yuko tayari kwa mapambano.Tangu mwanasiasa huyo alipondoka nchini kimya kimya wiki kadhaa zilizopita kwenda Ujerumani kwa matibabu, suala la afya yake limezua gumzo na kuibua mijadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, huku baadhi ikidai hali ni mbaya.




Akizungumza na waandishi wa habari jana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, Lowassa alisema alikwenda Ujerumani kuchunguzwa tatizo la macho ambalo lilikuwa likimsumbua. "Kumekuwa na maneno mengi kuwa naumwa na wengine wakisema ni mgonjwa sana lakini, yote hayo ni uongo,"alisema Lowassa na kuongeza: "Nilikuwa Ujerumani kwa ajili ya kuchunguzwa macho kama yana matatizo. Profesa wangu aliniambia niende ili kuangalia kama nahitajika kufanyiwa operation (upasuaji) lakini, ameniambia sina tatizo na afya yangu ni nzuri na pia mapigo yangu ya moyo yako 120/40 niko vizuri na sina presha."

http://maganga-resources.blogspot.com
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiriano, Cosmas Mwaisobwa
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), inaendelea na uhakiki wa majina na vielelezo vitakavyotumika kuwapeleka mahakamani wadaiwa sugu waliokaidi kurejesha madeni yao ya mikopo waliyochukua wakati wanasoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiriano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa, alisema kwa sasa kinachofanyika ni ukusanywaji wa taarifa zitakazotumika katika ufunguzi wa kesi pamoja na mashitaka kwa wale wote ambao hawajarejesha madeni.

“Kwa sasa tunakusanya vielelezo vya kutosha, hatuwezi kukimbilia mahakamani pasipokuwa na udhibitisho wa kutosha, tunayakusanya majina pamoja na taarifa zao ili tuweze kuwafahamisha kuwa tunawafungulia mashitaka,” alisema Mwaisobwa. HESLB ilitoa  notisi ya siku 21 kuanzia Januari 19, 2012 kwa wadaiwa wote wawe wamejitokeza na kufika ofisi za bodi. Kwa mujibu wa bodi hiyo, hadi sasa muda huo umeshapita na hakuna waliojitokeza, hivyo wameamua kuwafungulia mashitaka mahakamani.

http://maganga-resources.blogspot.com
  Vijembe na tambo vyatamalaki
  Nassari aendelea kuwelewa mikono
Mgombea ubunge Arumeru  (Chadema), Joshua Sumari,

Kampeni za kusaka ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Aprili mosi mwaka huu, sasa zimegupigwa na tambo za wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku vijembe vikitawala.


Timu ya wabunge wa CCM ilikishambulia Chadema kuwa hakina uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi wa Arumeru Mashariki kutoakana na kutokuwa na serikali. Wabunge hao Livingstone Lusinde (Mtera), Suleiman Said Jafo, (Kisarawe) na Lekule Laizer (Longido) walitoa shutuma hizo katika mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa CCM, Sioi Sumari, katika Kata ya Mbuguni.

Lusinde aliwaambia wananchi waliohudhuria  mikutano katika vijiji vya Msitu wa Mbogo na  Shambarai kuwa ilani ya maendeleo inayotekelezwa ni ya CCM ambacho ndicho chenye serikali. “Wana-Arumeru mchagueni Sioi ndiye anaweza kusikilizwa na serikali, angalieni sana wanakuja kuwadanganya muichukie CCM, nawashauri mtuchagulie Sioi ndiye anayeweza kusikilizwa na Rais wenu,” alisema Lusinde aka Kibajaj.



Alisema kuwa Jimbo la Arumeru Mashariki madiwani wote wanatokana na CCM, hivyo  kuchagua mbunge wa chama kingine kutawarudisha nyuma  katika harakati za kutafuta maendeleo. Aliwataka wasikubali kupandikiziwa chuki na hasira na kumnyima mgombea wa CCM kura kwani hiyo ni mbinu chafu inayotumiwa na Chadema kujinufaisha kisiasa.

“Tunajua wanapita kueneza chuki dhidi ya CCM, lakini najua wana-Arumeru Mashariki hamtakubali kurubuniwa na kukubali kumpigia kura mgombea tofauti na CCM, naomba muwashauri na wale ambao hawapo katika hadhara hii,” alisema Lusinde. Kwa upande wake, Jafo aliiponda Chadema kwa kueneza propaganda za upotoshaji ukweli wa mambo hasa kwa kueneza kuwa CCM ni cha wazee, madai aliyosema si ya kweli. “Hawa watu hawana sera, hebu angalia wabunge waliopo hapa yupi mzee nawashauri muwapuuze, CCM imejaa vijana simnatuoana hapa,” alisema na kuongeza: “Hawa wamekosa hoja, sasa wanapandikiza chuki, CCM ndicho kinaweza kuwatoa hatua moja kwenda mbele katika maendeleo.”

Naye Laizer aliwataka wakazi wa jimbo hilo kutorudia makosa waliyofanya mwaka 1995 ya kuchagua mbunge wa upinzani. “Naamini bado hamjasahau kosa mlilowahi kufanya la kuchagua Mbunge wa upinzania. Je, mlipomchagua mlimwoana hapa?” alihoji na kuongeza: “Sasa nawasihi mpeni kura zenu Sioi.”
Alisema  kuwa  amekuwa mbunge kwa kipindi kirefu na kwamba wabunge wa upinzani hawahudhurii vikao vya maendeleo katika ngazi ya mkoa. “Mfano ni kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), hawahudhurii na mfano ninaowapa ni Jimbo la Arusha, Mbunge wa jimbo hilo hajawahi kuhudhuria kikao hicho toka achaguliwe, hawana nia ya dhati hawa,” alisisitiza Laizer.

Akijinadi, Sioi Sumari aliwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua ili ashirikiane nao kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili. “Nimepita hapa wakati wa kura za maoni, tumezungumza nanyi, lakini sasa ninaomba mnipe kura ili tupambane pamoja kutatua kero mlizonazo zile zitakazokuwa juu ya uwezo wetu nitazipeleka mbele,” alisema.

MJANE WA KIRILO AMBARIKI NASSARI
Wakati wabunge wa CCM wakisaka kura kwa Sioi, jana mjane wa mtetezi wa haki za Wameru kabla ya Uhuru wa Tanganyika, kutoka Meru, Japhet  Kirilo, amembariki mgombea wa Chadema, Joshua Nassari kwa kumshika kichwani na kumtaka kutetea na kulinda haki za Wameru kama alivyofanya mumewe. Mjane huyo, Nderetwa Kirilo (85), kizungumza nyumbani kwake katika Kata ya Poli, baada ya kumbariki Nassari, alisema kuwa alimpa baraka hizo bila kujali anatoka chama gani, bali anaamini kuwa ataleta maendeleo kwa watu wa Meru.

“Mimi mume wangu aliyezaliwa mwaka 1921 Mzee Kirilo alishirikiana na Nyerere na wakati mwingine kulala hapa kwangu, wakiwa katika harakati za kudai uhuru wa Taifa letu na pia Wameru walichangisha fedha walizoweka ndani ya chungu maalum na kumwezesha mume wangu aliyeacha kazi ya udaktari na kwenda Umoja wa Mataifa kudai haki ya ardhi ya Wameru,” alisema Mama Kirilo.

Alisema kuwa mumewe alikuwa mwanaharakati wa siasa ambaye alithubutu kuacha taaluma yake na kuingia katika ulingo wa siasa kwa kutetea watu wa Meru, ambao walimchangia kwa moyo mmoja na kupata nauli ya kwenda Umoja wa Mataifa kudai ardhi ya Wameru. “Sasa niliposikia huyu kijanja wetu amejitokeza katika siasa na kugombea nafasi hii ya kutuwakilisha, mimi nambariki Mungu amtangulie ili akienda bungeni aweze kuwa chachu kwa kutetea ardhi ya Wameru,” alisema Kirilo.

Nassari alimshukuru bibi huyo na kumuahidi kuendeleza aliyoasisi Mzee Kirilo, aliyefariki dunia mwaka 1997 kwa kutetea haki za Wameru hasa ardhi. “Bibi mimi sitakuwa msaliti, naomba unitetee na kuniombea kwa Mungu ili anibariki nitakapopata ubunge,” alisema Nassari.

FEDHA ZA TASAF
Akiomba kura katika Kata ya Songoro kwenye kijiji cha Sura na kijiji cha Ndatu, Nassari alisema kuwa endapo atachaguliwa atawatetea bungeni wananchi wa eneo hilo kuhakikisha fedha zilizoliwa na wajanja za Mfumo wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Sh. million 26 za ujenzi wa barabara ya  Nkoakirika hadi kijiji cha Sura zilizotolewa mwaka jana zinapatikana na kufanya kazi iliyokusudiwa. Nassari alisema kuwa kijijini hapo kuna mradi wa maji toka mwaka 1992 ambao hata hivyo, hadi leo haujatekelezwa na hakuna maelezo yoyote yanayotolewa, hivyo aliomba kupewa ridhaa ya kuwa mbunge ili akawatoe panya katika halmashauri ya Arumeru wanaotafuna fedha za umma.

Meneja wa Kampeni, Vincent Nyerere, alisema anaishangaa serikali kwa kupeleka magari ya programu za maji kwa kila wilaya na mikoa, lakini hakuna maji yanayopelekwa kwa wananchi na kuahidi kuwa ikiwa Chadema kitashinda na kushika dola, watauza magari yote ili kupeleka maji kwa wananchi. Nyerere ambaye ni Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), alitahadharisha Polisi kuwa makini na kikosi cha vijana wa CCM kutoka Musoma na basi maalum kwa lengo la kuleta vurugu kwenye kampeni hizo, na kwamba wao hawahitaji vurugu kwa kuwa ushindi upo kwao.

Mbunge wa Karatu (Chadema), Mchungaji Israel Natse, aliwaomba wananchi hao kuzingatia maadili ya kabila lao kwa kuchagua mbunge anayeyafuata. Mchungaji Natse alisema kuwa anaishangaa serikali kusisitiza sera ya Kilimo Kwanza wakati utekelezaji wake ni hafifu na kuwapelekea wakulima pembejeo za kilimo wakati msimu wa kilimo ukiwa umepita.

SOURCE: NIPASHE
http://maganga-resources.blogspot.com
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu nchini (HESLB) imetangaza orodha ya majina ya wanavyuo wa Elimu ya juu nchini walishinda rufaa ya mean test walizokuwa wamepangiwa awali. Orodha hiyo iko katika makundi mawili la waombaji wapya 9wale wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea. Akitanagaza majina hayo, mkurugenzi wa bodi ya mikopo alisema kuwa hayo ni majina ya waombaji waliofanikiwa katika rufaa zao walizoomba. 

Aidha, aliongezea kuwa, kutokana na ufinyu wa bajeti bodi ya mikopo imeshindwa kupitisha maamuzi juu ya wanafunzi wale ambao hawakupata kabisa mikopo kutokana na ufinyu wa bajeti au sababu nyingine kwa mwaka wa masomo wa 2011/2012. "Kwa taarifa hii, bodi inasikitika kuwataarifu wote waliokata rufaa na majina yao hayajaonekana kwenye hii orodha kujihesabu kuwa hawajafanikiwa.

BONYEZA LINK HAPA CHINI USOME ORODHA YA MAJINA

MWAKA WA KWANZA                                WANAFUNZI WANAOENDELEA
(First year students)                                    (Continuing Students) 

http://maganga-resources.blogspot.com
Moja ya ndege za BAE
Kampuni ya kuuza vifaa vya kijeshi ya BAE Systems itatoa takriban £29.5m kwa miradi ya elimu nchini Tanzania kufuatia makubaliano na Taasisi ya Kupambana na ufisadi ya Uingereza (SFO). BAE ilipigwa faini ya £500,000 mwaka 2010 kwa kushindwa kutunza rekodi zake za malipo iliyofanya kwa mshauri wake.
Malipo hayo yalitolewa kununua rada ya kijeshi kwa Tanzania kwa gharama ya £28m. Kampuni hiyo ya BAE sasa imethibitisha makubaliano ambayo yatatumika kusaidia watanzania kama ilivyoafikiwa
.
Itanunua vitabu vya kiada kwa shule 16,000 vya masomo muhimu ya Kiswahli, Kiingereza, Hisabati na Sayansi. Fedha hizo pia zitatumika kuwapatia miongozo walimu na mwongozo wa muhtasari wa masomo kwa waalimu wote 175,000 wa shule za msingi, na muhtasari yenyewe, kampuni hiyo ya ulinzi imesema.


Taasisi ya SFO ilisema makubaliano hayo yalikuwa ya kwanza na ya aina yake, lakini ilikosolewa na jaji aliyetoa uamuzi wake kwa kampuni hiyo miaka miwili iliyopita. "Makubaliano haya ni ya kwanza kwa SFO ambayo iliratibu kutumia mfumo wa sheria za Uingereza,’ mkurugenzi wa SFO Richard Alderman alisema. 'hatma ya jambo lenyewe' "Tumefurahi kuwa hatimaye tumefikia mahali tunaweza kutoa malipo kwa serikali yaTanzaniana kufikia tamati ya suala hili." BAE ilisema.

BAE iliafikiana na SFO mpango huo mwaka 2010. Ilikubali kulipa faini ya na gharama ya £225,000 kwa SFO – na faini ilikokotolewa kutoka £30m iliyotoa kwa watanzania kumaliza kesi hiyo.

Wakati huo jaji wa mahakama ya Southwark Crown alikosoa makubaliano hayo kati ya SFO na BAE. "Muundo wa makubaliano hayo unaweka shinikizo la kimaadili kwa mahakama kuifanya faini hiyo iwe kwenye kiwango cha chini kwa ajili ya maandalizi ya juu. " alisema Justice Bean, aliyeongeza kuwa alikuwa kwenye shinikizo la kuiweka faini ya mahakama kuwa ya chini.

Pia alikosoa sehemu nyingine ya makubaliano ambayo alisema yalimpa mjumbe yeyote wa kampuni ya BAE Systems "kinga kwa makosa yote yaliyofanywa nyuma yawe yamewekwa wazi au la". Kampuni hiyo ililipa £7.7m kwa kampuni mbili zinazomilikiwa na mfanyabiashara Shailesh Vithlani kabla hata ya kushinda zabuni yenyewe ya kununua rada.

http://maganga-resources.blogspot.com
Rais mstaafu Benjamin Mkapa
ASEMA VINCENT NI MDOGO WAO, ATAKA TUHUMA ZINGINE AJIBU MWENYEWE
Waandishi wetu, Dar, Arumeru 
MADARAKA Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ameibuka na kuthibitisha kuwa Mbunge wa sasa wa Musoma mjini (Chadema), Vincent Nyerere ni mdogo wao na mwanafamilia hiyo, kwani ni mtoto wa baba yao mdogo, Josephat Kiboko Nyerere.

Kauli ya Madaraka imekuja siku chache baada ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, kudai kwamba hamtambui mbunge huyo kuwa ni miongoni mwa familia ya Mwalimu Nyerere kwani katika kipindi chote alichofanya kazi na Mwalimu, hakusikia jina hilo.

Jumatatu ya wiki, akizindua kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, Mkapa aliuambia umati uliohudhuria kwamba hakuwahi kusikia kama kulikuwa na mtoto wa familia hiyo aliyekuwa akiitwa Vincent Nyerere.

Kauli hiyo ilipingwa vikali juzi na Vincent akisema si jambo la ajabu Mkapa kutomfahamu yeye kwasababu Mkapa si sehemu ya ukoo wao huku akimrushia kombora kwamba akiwa madarakani alishinikiza Mwalimu Nyerere kupelekwa Hospitali ya St Thomas, Uingereza, kinyume na matakwa ya familia yao na wakati huo huo, daktari wake Profesa David Mwakyusa alijua maradhi ya mwasisi huyo wa taifa.

Raia mmoja wa Uholanzi, Marise Koch, amemfanyia kitendo cha udhalilishaji Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Marera iliyopo kata ya Rhotia Wilayani Karatu mkoani Arusha kwa kumpiga vibao mbele ya wanafunzi na walimu wenzake.
 
Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na viongozi wa Idara ya Elimu Wilaya ya Karatu na Jeshi la Polisi, zinasema kutokana na udhalilishaji huo, raia huyo wa Uholanzi ameshafunguliwa jalada lenye namba KRT/RB/835/2012 katika kituo cha polisi Karatu kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli
  
OPERESHENI  ya kusafisha jiji la Dar es iliyotangazwa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli imeshika kasi baada ya tingatinga kubomoa vibanda vya biashara kando ya barabara ya Dar- Morogoro, eneo la Kimara jana.  Tukio hilo lilizua taharuki kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaomiliki mabanda hayo, ambao walihaha kuokoa mali zilizokuwa ndani, bila mafanikio.

Msimamizi mwandamizi wa operesheni hiyo, Hamis Abdul alisema kazi hiyo ni endelevu na kwamba baada ya kutoka Kimara, watahamia barabara ya Bagamoyo eneo la Tegeta huku akiwatahadharisha wafanyabiashara waliovamia maeneo hayo, kuhama mara moja.

Abdul aliwataka wafanyabiashara wote wanaofanya shughuli zao katika hifadhi za barabara kuondoka maeneo hayo kwa hiari yao kuepuka hasara ya kubomolewa mabanda yao. “Zoezi hili ni endelevu na kwamba baada tu ya kumaliza barabara hii ya Morogoro,  operesheni hii itahamia katika maeneo ya  Tegeta, kwa hiyo ningependa kutumia fursa hii kuwapa tahadhari wafanyabiashara waliovamia  maeneo ya barabara kuondoka kabla hatujafika huko,” alionya. Wenye vibanda
Maafisa wa jeshi la Marekani wamebainisha kuwa askari wa jeshi hilo ambaye anatuhumiwa kuwaua raia kumi na sita wa Afghanistan mwishoni mwa wiki, ameondolewa nchini humo.
Leon Panetta
Mwanajeshi huyo huenda akahukumiwa kifo

Askari huyo ambaye bado hajatajwa jina amesemekana kupelekwa Kuwait. Maafisa hao wamesema hatua za kisheria dhidi ya askari huyo, kwa sasa zitaendeshwa nje ya Afghanistan.

Waathirika wa shambulio hilo tisa kati yao wakiwa ni watoto, waliuawa kwa kupigwa risasi majumbani mwao, usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita.
Kuondolewa kwa mwanajeshi huyo huenda kukachochea hasira kali nchini Afghanistan hasaa baada wabunge nchini humo kutaka afunguliwe mashataka nchini mwao.

Lakini ilikuwa wazi hilo halingetendeka. Kulingana na sera za Marekani mwanajeshi wawake wowote anayepatikana na hatia sharti afunguliwe mashataka kulingana na sheria za jeshi lake. Hata hivyo mwanajeshi huyo bado hajafunguliwa mashataka na kwa hivyo kufikia sasa bado hajajulikana. Kulingana na maafisa ikiwa atakuwa anahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kubainisha ikiwa ana akili timamu, basi itachukuwa muda kabla ajulikane au hata kufunguliwa mashataka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma
WIKI moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuagiza Jeshi polisi kuwafukuza kazi askari wote wasio waadilifu, jeshi hilo mkoani Kilimanjaro limewafukuza kazi polisi wake watatu kwa tuhuma za kufanya shughuli za udalali na kuuza mali ya mdaiwa.

Polisi waliofukuzwa kazi ni mwenye namba D.3289 Sajenti Joseph aliyekuwa dereva wa mkuu wa kituo (OCS), F.3677 PC Esebius wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID) na polisi wa kawaida mwenye namba F.6620, PC Johnson.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma alithibitisha kufukuzwa kazi kwa askari hao akisema hatua hiyo imetokana na kugeuka madalali na kuuza mali ya mfanyabiashara mmoja wa Rombo, Genes Shayo (34).

Ilidaiwa kuwa polisi hao waliuza mali ya mfanyabiashara huyo bila ya ridhaa yake wala kuwepo wakati wa mauziano hayo kitendo kilichodaiwa kuwa kilisababisha mfanyabiashara huyo kunywa sumu na kupoteza maisha usiku wa Februari 24, mwaka huu.
MKURUGENZI wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi, amesema hadi sasa ni vigumu kufahamu atakapopeleka mahakamani jalada la kesi kwa watu wanaotuhumiwa kutoa taarifa kwamba ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, unatokana na kulishwa sumu. “Ni vigumu kusema ni lini itapelekwa mahakamani... bado tunalifanyia kazii," alisema Feleshi akisisitiza uchunguzi wao ukikamilika wataamua kuipeleka mahakamani au la, kulingana na kanuni na taratibu za ofisi hiyo.

Jalada hilo lilifika kwa DPP likitoka kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, ambaye alisema uchunguzi wa polisi umebaini Dk Mwakyembe hajaugua kwa sababu ya kulishwa sumu, hivyo waliohusika kutoa kauli hizo watawachukulia hatua.

Ramani ya Zambia
Ramani ya Zambia
             
Chama tawala hapo zamani nchini Zambia cha MMD kimepokonywa hadhi yake ya kisheria kwa kushindwa kulipa ada inayohitajika na vyama vilivyosajiliwa kwa kipindi cha miaka 20 takriban dola $75,000 (£50,000).
Msajili wa mashirika amesema kua Chama hicho cha MMD kimefutwa kutoka daftari la usajili kwa kushindwa kulkipa ada chini ya sheria.

Chama hicho kimekanusha kua kinadaiwa na kusema kitakata rufaa kwa kile lililotaja kua shambulio dhidi ya demokrasi. Endapo uwamuzi huu utazingatiwa, chama cha MMD kitapoteza viti vyake katika bunge. 


Hiki ni mojapo ya vyama vikongwe vya kisiasa kilichoingia madarakani mnamo mwaka 1991 katika uchaguzi wa kwanza ulioshirikisha vyama vingi.
Mwaka jana kilijitokeza kua chama kikubwa cha upinzani kikiwa na viti 53 na baada ya hapo kikashindwa na chama cha Patriotic front cha Rais Michael Sata aliyeshinda uchaguzi na kushika hatamu za uongozi wa Zambia.
BENKI Kuu ya Tanzania imeongeza muda wa mwaka mmoja kwa wateja wa benki zote nchini kuboresha taarifa zao kuanzia kesho Machi 15, 2012 hadi Machi 14, 2013. Benki na taasisi zote za fedha zimejulishwa kuzingatia kikamilifu agizo hili. Agizo la awali lilitamka kwamba muda wa kuboresha taarifa za wateja wa benki ungelimalizika leo. Mwaka jana (2011) Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo, alitoa kipindi cha muda wa mwaka mmoja kuanzia Machi 15, 2011 hadi Machi 14, 2012 kwa ajili ya zoezi hilo. Hii ilikuwa ni kuziwezesha benki zote kuzingatia kanuni zilizomo katika Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu.

Wakati huo huo, Benki Kuu ya Tanzania inawataka wananchi na wateja wa benki nchini kutimiza wajibu wao kwa kujaza fomu za taarifa zao ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kwa kushindwa kutimiza sharti hilo la kisheria. 

Imetolewa na Idara ya Uhusiano na Itifaki 
BENKI KUU YA TANZANIA 
Machi 14, 2012
http://maganga-resources.blogspot.com
Rais mstaafu wa awamu ya pili Mh B. W. Mkapa
VITA ya maneno, vijembe na kejeli kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha imeanza.Baada ya juzi Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kufanya uzinduzi wa kampeni za CCM na kuipiga vijembe CHADEMA, chama hicho jana kilijibu mapigo kupitia kwa Mbunge wa Msoma Mjini, Vincent Nyerere, ambaye ni Naibu Meneja wa Kampeni wa CHADEMA.

Akizungumza katika mikutano ya kampeni maeneo mbalimbali, mbunge huyo alishusha tuhuma nzito juu ya kile alichokiita ‘utata’ wa kifo cha Mwalimu Nyerere huku akihusisha na maamuzi ya Mkapa kung’ang’ania Mwalimu aende kutibiwa Uingereza baada ya kuanza kumkosoa juu ya sera za ubinafsishaji. Nyerere ambaye ni mmoja wa wanafamilia wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, akiwa amekulia katika familia hiyo, aliwaambia wananchi wa maeneo hayo kuwa umefika wakati sasa Mkapa atoke hadharani afafanue alikuwa na nia gani kumlazimisha Mwalimu Nyerere akatibiwe Uingereza wakati mwenyewe alikuwa amekataa, akisema kuwa ugonjwa uliokuwa unamsumbua tayari ulikuwa unajulikana na daktari wake, Profesa David Mwakyusa, alikuwa tayari akimhudumia vizuri bila tatizo.
                               JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
                            Simu: 022-2121600 Faksi: 022-2113271 Tovuti: www.moe.go.tz
  TANGAZO KUHUSU NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013

NB: MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 30/04/2012.

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anatangaza nafasi za mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2012/2013 kama ifuatavyo:


(A) MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI
1. CHETI DARAJA A: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Aliyehitimu Kidato cha 4 kati ya mwaka 2009 hadi 2011 na kufaulu katika kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 kwa mtihani uliofanyika katika kikao kimoja AU mwenye ufaulu wa masomo manne kwa kiwango cha C au zaidi (masomo yanayofundishwa katika shule za Msingi) kwa mitihani iliyofanyika katika vikao zaidi ya kimoja;


(b) Aliyehitimu Kidato cha 6 na kukosa sifa za kujiunga na Stashahada ni sifa ya nyongeza.
Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya ‘Mathematics, Biology, Physics, Chemistry and English‟.


2. CHETI (MICHEZO): MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Ufaulu wa Kidato cha 4 kwa kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 (Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya ‘Mathematics, Biology, Physics, Chemistry and English‟;
(b) Aliyehitimu Kidato cha 6 na kukosa sifa za kujiunga na Stashahada ni sifa ya nyongeza; na
(c) Mwenye uzoefu katika michezo ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).


3. CHETI (ELIMU YA AWALI): MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Aliyehitimu Kidato cha 4 kati ya mwaka 2009 hadi 2011 na kufaulu katika kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 kwa mtihani uliofanyika katika kikao kimoja; na
(b) Kuhitimu Kidato cha 6 ni sifa ya nyongeza.


(B) MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA CHETI
1. CHETI SAYANSI KIMU: MUDA WA MAFUNZO NI MWAKA 1
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya ualimu Daraja A;
(b) Uzoefu wa kazi ya ualimu usiopungua miaka 2;
(c) Aliyefaulu masomo ya Sayansi na Sayansi Kimu; na
(d) Aliyefaulu mtihani wa Kidato cha 4 kwa kiwango kisichopungua daraja la IV alama 28.


2. CHETI ELIMU MAALUM: MUDA WA MAFUNZO NI MWAKA 1
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya ualimu Daraja A;
(b) Uzoefu wa kazi ya ualimu usiopungua miaka 2;
(c) Aliyefaulu angalau somo moja la Sayansi katika mtihani wa Kidato cha 4;
(d) Aliyefaulu mtihani wa Kidato cha 4 kwa kiwango kisichopungua daraja la IV alama 28; na
(e) Mwalimu anayefundisha Elimu Maalum hata kama hana mafunzo rasmi ni sifa ya nyongeza(vithibitisho viambatishwe)..


(C) MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA
1. STASHAHADA YA UALIMU MASOMO YA SAYANSI, SAYANSI YA JAMII NA LUGHA : MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
Ufaulu wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari Kidato cha 1 hadi 4.
Masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari Kidato cha 1 hadi 4 ambayo ni; Mathematics, English, Kiswahili, History, Geography, Civics, Biology, Chemistry, Physics, Agricultural Science, Bookeeping, Commerce.


2. STASHAHADA YA UALIMU MICHEZO, MUZIKI, SANAA ZA UFUNDI NA SANAA ZA MAONESHO: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
Ufaulu wa mtihani Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja kwa kuzingatia masomo yafuatayo kwa kila kozi:
-Sanaa za Ufundi: masomo ya ‘Fine Art’ pamoja na ufaulu wa Kidato cha 4 masomo ya ‘Biology, History, Physics, English, and Civil Engineering’
-Sanaa za Maonesho: masomo ya ‘Literature in English, Kiswahili, Geography and History;

-Muziki: masomo ya ‘English, Kiswahili, Music, Physics, Geography and History’; na
-Elimu kwa Michezo: masomo ya Biology, Chemistry, Physics, English’ na Kiswahili.


3. STASHAHADA YA UALIMU UFUNDI: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwenye cheti cha FTC kutoka vyuo vya Ufundi (Arusha, Mbeya, Dar es Salaam) au sifa zinazolingana; na
(b) Mwenye umri usiozidi miaka 35.


4. STASHAHADA YA UALIMU KILIMO: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
Ufaulu wa mtihani Kidato cha 6 kiwango kisichopungua “Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja katika somo la ‘Agricultural’ Science na ‘Biology’ au ‘Chemistry’.


5. STASHAHADA YA UALIMU BIASHARA: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo ya ‘Accounts and Commerce’.


6. STASHAHADA YA UALIMU SAYANSI KIMU: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kiwango kisichopungua ‘Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja katika masomo ya ‘Biology, Chemistry and Nutrition’.


(D) MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA STASHAHADA
1. STASHAHADA YA UALIMU MASOMO YA SAYANSI, SAYANSI YA JAMII NA LUGHA: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu mwenye Cheti cha Ualimu Daraja A na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili; na
(b) Ufaulu wa mtihani Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari (Kidato cha 1 hadi 4). Masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari ni; Mathematics, English, Kiswahili, History, Geography, Civics, Biology, Chemistry, Physics, Agricultural Science, Bookeeping, Commerce.


2. STASHAHADA YA UALIMU ELIMU MAALUM: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi au Sayansi ya Jamii na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili ;
(b) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari;
(c) Mwalimu anayefundisha watoto wenye mahitaji maalumu (wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili nk) ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).


3. STASHAHADA YA UALIMU SAYANSI KIMU: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu mwenye Cheti cha Ualimu Daraja A;
(b) Mwalimu mwenye Cheti cha ualimu Sayansi Kimu; na
(c) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo ya ‘Biology, Chemistry and Nutrition’.


VIAMBATISHO/ MAELEZO MUHIMU
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu waambatishe vielelezo vifuatavyo:
(i) Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV na cha VI;
(ii) Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stahshahada (kwa Walimu kazini);
(iii) Barua za Walimu kazini zilizopitishwa na Waajiri;
(iv) Sifa zilizoelekezwa kwa kila kozi ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya ualimu katika vyuo vya ualimu vya Serikali na Vyuo Visivyo vya Serikali;
(v) Wahitimu wa Kidato cha 4 mwaka 2011 na Kidato cha 6 mwaka 2012 walioomba kupitia „Sel forms‟ wanatakiwa kutuma maombi upya kwa barua;
(vi) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu yatatolewa kwenye Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
(vii) Barua za kujiunga na mafunzo zitatolewa na chuo atakakopangwa mwombaji kwa kutumia anuani ya yake; na
(viii) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, Ofisi za Makatibu Tawala (M) na Vyuo vya Ualimu.
MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 30/04/2012.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)

http://maganga-resources.blogspot.com
Stesheni ya Kigoma
Na mwandishi wetu.
Wazazi wa wanafunzi  wa shule za sekondari mbalimbali mkoani Kigoma wamelalamikia suala la wanafunzi kulipa ada na michango mbalimbali kupitia benki. Wakiongea na mwandishi wetu walisema kuwa hawana nia ya kupingana na maendeleo bali kwanza wazazi wa wanafunzi hao hawajaandaliwa vizuri kuhusu mabadiliko hayo na pia wanafunzi wanatumia muda mwingi katika kupanga foleni benki ili kuweza kulipa michango yao. 

Aidha mwandishi wa habari hii aliweza kuwaona baadhi wanafunzi wakikabiliwa na adha hiyo huku wenzao wakiwa madarasani. "Baba ameenda kazini na mama anasema mambo ya benki hayajui hivyo nimelazimika kuja kulipa mwenyewe benki", aliongea mwanafunzi aliyehojiwa.
Salva Kiir na Omar al Bashir
Viongozi hawa watakutana tena mjini Juba
    
Makubaliano hayo kati ya wawakilishi kutoka jamhuri ya Sudan and ile ya Sudan Kusini ni njia moja ya kuimarisha uhusiano kati ya majirani hawa ambao ulikuwa unazorota kwa kasi.
Nchini zote mbili zimekubaliana kuwa raia wao wataruhusiwa kuishi, kutembea na hata kuwekeza au kununua mali bila vikwazo vyovyote.
Makubaliano haya yatakuwa afueni kwa raia wa sudan kusini kama nusu milioni hivi, ambao bado wanaishi Sudan.
Utawala mjini Khartoum ulikuwa umetangaza kuwa kwanzia mwezi ujao, watalazimika kubadilisha uraia wao au watachukuliwa kama raia wa kigeni.
Mpatinishi mkuu katika mazungumzao hayo aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, amesema Rais Salva kiir na mwenzake Omar Al Bashir watatia saini makubaliano hayo katika sherehe rasmi itakayo fanyika Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.
Hata hivyo suala la mafuta ambalo limezua utata zaidi kati ya majirani hao bado halijatatuliwa.
Wawakilishi wa pande zote wamekubaliana kuhusu kutengeza mipaka kati yao.
Suala la kutokuwepo na alama za mipaka limekuwa likichochea mzozo kati ya nchi hizo mbili.
Hatua hii nu muhimu sana katika ile hali ya kuondoa hofu ya kuzuka kwa vita kati ya majirani hawa.
Hata hivyo wadadisi wa siasa wanasema bado ni mapema sana kusheherekea kwani mara kadhaa makubulaiano yaliotiwa sahihi hayajafuatiwa na utekelezaji.

http://maganga-resources.blogspot.com

Thomas Lubanga katika mahakama ya ICC

Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC iliyoko the Hague, imempata na hatia ya uhalifu wa kivita mbabe wa zamani wa kivita katika Jamuhuri Ya Kidemokrasia ya Congo Thomas Lubanga.
Hukumu hiyo ndiyo ya kwanza kutolewa na mahakama ya ICC tangu kubuniwa kwake zaidi ya muongo mmoja uliopita. Hata hivyo mahakama itaamua baadaye hii leo adhabu atakayopata Lubanga.
Lubanga alipatikana na hatia ya kuwasajili watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na mitano kama wanajeshi wake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya congo.
Lubanga pia alisemekana kuwa kiongozi wa kundi la waasi wakati wa makabiliano ya kikabila katika eneo lenya utajiri wa dhahabu nchini humo.
Upande wa mashtaka ulimtuhumu Lubanga kwa kutumia watoto kama watumwa wa ngono, walinzi wake na wapiganaji wake.
Katika uamuzi uliopitishwa kwa kauli moja, majaji watatu waliokuwa wanasikiliza kesi dhidi ya Lubanga, walisema kuwa ushahidi dhidi ya Lubanga ulithibitisha kuwa kundi la waasi lilioongozwa na Lubanga pia linapaswa kuwajibishwa kwa makosa ya kusajili watoto kama wapiganaji waliopigana kwenye msityari wa mbele.
Lubanga, aliyekamatwa mwaka 2005, huenda akahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kupitisha hukumu ya kunyongwa.

http://maganga-resources.blogspot.com
Muingereza ambaye mwili wake mzima umepooza sana kiasi cha kutaka daktari amuue amepewa idhini apeleke kesi yake katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo.
Tony Nicklison, mwenye umri wa miaka 58, anataka daktari yeyote anayekubali maombi yake asikabiliwe na mashtaka ya mauaji.
Wizara ya Haki ya Uingereza inapinga ombi hilo la Bwana Nicklison. Bwana Nicklson alipooza mwaka 2005 na wakati huu anakabiliwa na maradhi yajulikanayo kama "locked in syndrome" ambapo mwili wake umepooza lakini akili yake ni timamu.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya kisheria anasema kesi hiyo itajadili maswala yanayozidi mtu kusaidiwa kujiua, kwa sababu Bwana Nicklson anataka mtu wa kumwua sio wa kumsaidia kujiua kwa sababu hana uwezo

http://maganga-resources.blogspot.com
Kiongozi wa zamani wa waasi, huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Thomas Lubanga Dyilo leo hii atajua hatima yake kufuatia mashitaka kadha yanayomkabili, yakiwemo ya kuwatumia askari watoto katika jeshi lake.
Thomas Lubanga
Hukumu hiyo inasubiriwa kwa hamu DR Congo
Hii itakuwa hukumu ya kwanza tangu kuzinduliwa kwa mahakama ya Kimataifa ya kushughulikia makosa ya Uhalifu wa Kivita ICC.
Bw Lubanga anatuhumiwa kuongoza wapiganaji wa kabila la Wahema katika makabiliano ya wenzao Walendu katika vita vilivyotokea miaka kumi iliopita katika mkoa wa Ituri.
Muasi huyo amekanusha mashtaka yanayomakabili na anasisitiza kuwa yeye alikuwa mwanasiasa na sio mpiganaji.
Makundi yakutetea haki za binadamu yanasema utafiti wao umeonyesha kuwa zaidi ya watu elfu 60 waliuawa katika vita hivyo katika eneo la Ituri ambapo Thomas Lubanga alikuwa na ngome yake.
"Utafiti wetu unaonyesha kuwa uhalifu wa kivita ulitendeka, wanawake walibakwa, watu waliteswa na wengine walizuiliwa bila kufanya makosa yoyote wakati wa vita hivyo vya kikabila. Ni matumaini yetu kuwa hukumu ya leo itakuwa ishara kuwa haki itatendeka" alisema Bi Anneke Van Woudenberg wa shirika la Human Rights Watch.
Thomas Lubanga ndio kiongozi aliyefunguliwa mashataka lakini mwenzake Jenerali Bosco Ntaganda bado hajachukuliwa hatua zozote na anatumikia jeshi la DR Congo.
Kesi hii imedumu kwa muda mrefu na hukumu hii inasubiriwa kwa hamu ni wakaazi wa Ituri ambao bado wanamakovu ya vita hivyo.

http://maganga-resources.blogspot.com
Jeshi la Israil limekuwa likiendelea na mashambulio ya ndege dhidi ya Wapalestina katika Kanda ya Gaza, kwa siku ya tatu mfululizo.
Mji wa Gaza ukishambuliwa na ndege za Israil
Walioshuhudia matukio hayo wanasema mtoto wa kiume wa miaka 12 aliuwawa karibu na kambi ya wakimbizi ya Jabaliya, na kwamba watu wengine walijeruhiwa katika shambulio la pili dhidi ya mji wa Gaza.
Idadi ya Wapalestina waliokufa sasa inakaribia 20; katika mashambulio makubwa kabisa kutokea Gaza kwa muda wa mwaka.
Wapiganaji wa Kipalestina nao wamerusha makombora dhidi ya Israil.
Mawaziri wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu wanaokutana mjini Cairo, wameishutumu Israil kuwa inazidisha utumiaji nguvu.
Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya zimeeleza wasiwasi na zimesihi utulivu.

http://maganga-resources.blogspot.com

watoto wa Uganda
Watoto Uganda, wanakumbwa na ugonjwa usiojulikana chanzo wa 'kusinzia
'
Uganda imefungua vituo vya afya vya kwanza maalum kwa kusaidia maelfu ya wattoto ambao wana dalili za ugonjwa ambao haujajulikana chanzo chake wa 'kusinzia.’
Vituo hivyo vilivyo kaskazini mwa nchi, ambako ugonjwa huo umeenea, vinakusudiwa kudhibiti dalili mbaya za ugonjwa huo.
Chanzo cha ugonjwa huo hakijajulikana lakini unawapata watoto pekee, wanaoshambuliwa na dalili za kudumaa kiakili na kimwili na kusinzia.
Kuna taarifa za ugonjwa huo kuwa upo nchi za Sudan Kusini na Tanzania.

Maiti za watu wanaoshukiwa kuuawa na mwanajeshi wa Marekani
Rais Barack Obama amesema mauaji ya raia kumi na sita wa Afghanistan yalitekelezwa na askari mmoja wa Marekani Jumapili iliyopita, yanaonyesha umuhimu a majeshi ya Marekani kuondoka nchini humo-- lakini ametahadharisha dhidi ya uamuzi wa kuharakisha kuondoka.
Bwana Obama amesema majeshi ya Marekani yataondoka Afghanistan katika utaratibu uliopangwa, ili yasiishie kurudi tena huko.

Akiulizwa kuhusu mauaji ya raia wa Afghanistan katika mahojiano ya televisheni mbalimbali za Marekani, Bwana Obama amesema mauaji hayo ni ya askari binafsi na wala sio kielelezo cha utendakazi wa majeshi ya Marekani kwa jumla.
Marekani inapanga kukabidhi shughuli za usalama kwa majeshi ya Afghanistan ifikapo mwaka 2014.
''Hatutaki kuchukua hatua za haraka. Tuna mamia ya watu wanaotupa ushauri. Tuna vifaa vingi ambavyo vinahitaji kuhamishwa...lazima tuhakikishe kwamba raia wa Afghanistan wanaweza kulinda mipaka yao na kuzuia kundi la Al Qaeda kurejea tena ..Kwa hiyo lazima tuchukue hatua kwa njia inayofaa'
Wachanganuzi wanasema tukio hilo halilitaathiri mikakati ya Marekani nchini Afghanistan.
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imesema Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila ana kesi ya kujibu katika kesi ya kuchapisha na kuusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo, ikiwa ni siku chache baada ya upande wa mashitaka kufunga ushahidi baada ya kuwaleta mahakamani hapo mashahidi watano.
Hakimu Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi wa upande wa serikali, amebaini kuwa Mchungaji Mtikila ana kesi ya kujibu na kwa maana hiyo mchungaji huyo maarufu kwa kukabiliana na kesi za uchochezi, atatakiwa kupanda kizimbani Aprili 11 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kujitetea.
Baada ya uamuzi huo, Mtikila ambaye hana wakili wa kumtetea na kuamua kujitetea mwenyewe, alidai kuwa anatarajia kuleta mashahidi 10 wa kumtetea katika kesi hiyo inayovuta hisia za wengi nchini.
Februari mwaka huu, Mtikila alikiri maelezo aliyochukuliwa na ofisa wa polisi kuwa ni yake na kwamba hana pingamizi nayo, hivyo mahakama iliyapokea kama kielezo cha upande wa mashitaka.
Kampuni ya Yahoo imeushtaki mtandao mkubwa wa kijamii Facebook juu ya ukiukwaji wa kanuni muhimu faragha, matangazo, na meseji. Yahoo ina kesi dhidi ya Facebook katika mahakama ya California, kwa shutuma kubwa ya kukiuka juu ya kanuni 10 zilizoanzishwa na waanzilishi Internet.

Yahoo katika kurasa 19 za mashtaka zilizojazwa katika Mahakama ya Wilaya ya Marekani kwa ajili ya Wilaya ya Kaskazini ya California, ameishtaki Facebook kukiuka kanuni katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na faragha, matangazo, na meseji.
Msemaji wa kampuni ya Yahoo wa California, bwana Sunnyvale, aliitaka mahakama katika San Jose kusitisha shughuli za Facebook zinazokiuka kanuni kusaidia kufanya tathmini za uharibifu usiyojulikana.

"Yahoo imewekeza rasilimali kubwa katika utafiti na maendeleo kwa miaka mingi, ambayo imesababisha uvumbuzi mbalimbali wa teknolojia na kuwa na hati miliki, makampuni mengine yana leseni," Alisema katika taarifa yake. "Teknolojia hizi ni msingi wa biashara yetu ambayo inahusisha zaidi ya watu 700m  kila mwezi na kuwakilisha roho ya uvumbuzi ambayo ni msingi wa Yahoo!” alisema.
HALMASHAURI  ya  Mji  Mpanda, Mkoa  mpya  wa  Katavi,  ipo  katika  mchakato wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo (Kua) kama moja ya vitega uchumi na kuboresha huduma muhimu kwa maendeleo ya jamii na uchumi.
Akizungumza kwenye kikao maalumu cha Baraza la Madiwani, Kaimu Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Mji Mpanda, Nzori Kinero,  alisema katika hatua za awali,  halmashauri hiyo imekiombea chuo hicho zaidi ya Sh3 bilioni kutoka taasisi za fedha.
Kinero alisema wakipata fedha za awali zitasaidia kuanzia uanzishwaji  wa  chuo hicho ambacho kinatarajiwa kujengwa mwaka huu.
"Effigies of President Obama were burned"
Militants in Afghanistan have launched an attack on a government delegation visiting the site where a US soldier killed 16 civilians. Two of Afghan President Hamid Karzai's brothers and several top security officials were in the delegation in Panjwai in Kandahar province. One Afghan soldier and three militants were killed, police said, and the delegation is heading back to Kandahar.
The US soldier said to have carried out Sunday's attacks is under arrest. The unnamed 38-year-old staff sergeant is being held at an undisclosed location. A senior Afghan official confirmed to the BBC that an attack "from several directions" had taken place on the delegation, which was there to meet villagers and tribal elders. Afghan forces returned fire.
The BBC's Bilal Sarwary in Kabul says officials reported a 10-minute gun battle during which Taliban fighters fired from a distance at a mosque where the delegation and civilians were taking part in a prayer service. Panjwai police said that in addition to the soldier killed, two other people, including an intelligence officer, were wounded.
One of Mr Karzai's brothers, Qayum, told the Associated Press news agency it appeared initially that the attack was not serious and the delegation "assumed that it was the national army that started to fire in the air". He said the delegation, which included Kandahar's governor and the minister of border and tribal affairs, was
Kumwelimisha mwanamke ni kuielimisha jamii nzima Airtel  Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo cha huduma Kwa jamii imezindua programu ya uwezeshaji kwa wasichana itakayo wawezesha wasichana wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 18 katika harakati za kufanikisha malengo yao ya baadae na kuwajengea uwezo wa kujiamini huku mafunzo hayo yakiwa yamebeba ujembe usemao “jenga maisha yako ya  baadae”

Akiongea wakati wa  ufunguzi wa Programu hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya wasichana  Canossa iliyopo Tegeta jijini Dar-es-Salaam Meneja Huduma kwa jamii Bi Tunu Kavishe alisema “Programu yetu ina lenga  kuwawezesha wasichana wote walioko shule za sekondari ikiwa ni muendelezo wa dhamira ‘Airtel Shule yetu’ ya kutoa elimu kwa jamii hasa   wasichana ili kuendeleza mahusiano yetu mazuri kati ya kampuni na wateja wetu waaaminifu.





A 12-year-old boy been killed in a fresh Israeli air strike on the Gaza Strip, bringing the death toll from Israeli attacks to 18 since Friday, according to Palestinian medical sources.
At least one more Palestinian was wounded in the early Sunday raid in the eastern part of the Gaza Strip, the sources said, after armed groups fired 100 rockets into Israel.
A Palestinian riding a motorcycle was killed and two others were wounded on Saturday afternoon in an Israeli air raid close to the southern town of Rafah near the border with Egypt .

Samira Ibrahim
The legal action brought by Samira Ibrahim has put a stop to virginity tests on female protesters
A military court in Egypt has acquitted an army doctor accused of carrying out forced "virginity tests" on women protesters, state media reports.

Ahmed Adel was cleared because the judge found contradictions in witness statements, Mena news agency said.
The case was brought by one of the women, Samira Ibrahim, who said the "tests" took place after they had been detained during protests last year.
Demonstrators are gathering to protest the ruling, the BBC's Jon Leyne says.
The practice drew an outcry after Ms Ibrahim and other women spoke out about their treatment following their arrest during a protest in Tahrir Square in March 2011 - weeks after the fall of President Hosni Mubarak.
They said they were forced by the Egyptian army, while in detention, to submit to a five-minute-long so-called virginity test by a male doctor.
The army initially denied such tests had taken place, but a senior general, speaking anonymously, later admitted that they had happened.
Ms Ibrahim launched a legal challenge to prevent such tests happening again, and Cairo's administrative court eventually ruled that the tests were illegal.
But she said, before the trial of Ahmed Adel, that witnesses she hoped would speak in her defence had changed their story at the last minute, our correspondent reports from Cairo.
According to Mena, the judge said he made the ruling "from what has been proven in documents and based on my conscience," adding that he had "not been subjected to any pressures".

http://maganga-resources.blogspot.com



Emperor Akihito: "We shall never forget those who gave their lives in rescue missions"
Japan is marking the first anniversary of the devastating earthquake and tsunami which struck the north-eastern coast, leaving 20,000 dead or missing.
The magnitude 9.0 quake, Japan's most powerful since records began, also triggered a serious nuclear accident at the Fukushima Daiichi nuclear plant.
Thousands of people were evacuated as radiation leaked from the plant.
There were memorial services, and a minute's silence was observed at the moment the quake hit, 14:46 local time.
The main memorial ceremony was held at Tokyo's National Theatre, attended by Japan's Emperor Akihito, Empress Michiko and Prime Minister Yoshihiko Noda.
"We shall not let our memory of the disasters fade," the 78-year-old emperor said in a brief televised address.
"I hope all the people will keep the victims in their hearts."
Glasgow street where boys kick football

 Independence will give Scotland the powers it needs to get rid of poverty and deprivation, deputy SNP leader Nicola Sturgeon will say later.
Scotland's deputy first minister will attack "heartless" UK government welfare reforms at her party's spring conference, in Glasgow.
She will say the changes are punishing the elderly and vulnerable.
Ms Sturgeon will seek to contrast the policy with an SNP vision to get people off benefits for the "right reasons".
The Westminster government says its UK-wide welfare reforms will save billions of pounds, by replacing disability living allowance with a personal independence payment and bringing in a single, universal credit.
But the SNP says the move will hit some of the people most in need of help.
Ms Sturgeon, also Scotland's health secretary, will tell the last day of the SNP conference that the Holyrood government has shown what can be achieved with the current devolved powers.
BIASHARA huria imezua mengi. Hali kadhalika Sayansi na Tekenolojia nayo, imeleta mengi. Katika kuwaondolea kero  wanawake wenye matiti yaliyosinyaa hapa nchini, wataalamu kutoka China wameanza kutoa huduma ya kunyanyua matiti hayo kwa kutumia mashine maalumu.
Wachina wamejipatia umaarufu katika kuleta bidhaa mbalimbali hapa nchini, zikiwamo za kuongeza nguvu za kiume, kupunguza uzito, kuotesha nywele, kujichubua (kumfanya mtu mweusi awe mweupe), kuongeza makalio nk.
Huduma hiyo ya kusimamisha matiti yaliyolala, imeanza kutolewa katika Saluni ya Blue Palace, iliyopo nyuma ya Shule ya Mapambano, Sinza jijini Dar es Salaam.
Haikuwa rahisi kuweza kuamini kuwa vitu kama hivi vinaweza kupatikana Tanzania. Mwananchi Jumapili lilifunga safari mpaka kwenye saluni hiyo inayomilikiwa na Sarafina Mtweve, kujionea jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.
Mbali na meneja wa saluni hiyo, Trust Mwembe, pia alikuwepo mtaalamu kutoka China aitwaye, Ciisy Pang, ni binti wa miaka 23 tu, lakini anasema kwa miaka minne amefanya kazi hiyo na kuwasaidia wanawake mbalimbali waliokuwa wakikerwa na matiti yaliyolegea au kuanguka.
Pang na kundi lake wanatoa huduma hii kwa gharama ya Sh150,000 kwa kuanzia, ingawa wanahisi gharama hizo zitapanda katika siku chache zijazo.
 Jinsi matiti yanavyosimamishwa