March 14, 2025
 

HABARI MPYA LEO  

NAFASI ZA KAZI

SENIOR PLANNING OFFICER      Qualifications: Bachelor’s Degree in Economics, Statistics, Planning, Bu...

Published by Admin

ACADEMIC NEWS AND SELECTION

TUMAINI UNIVERSITY MAKUMIRA (TUMA) FIRST LIST OF ADMITTED STUDENTS INTO VARIOUS PROGRAMMES AT (TUMA) 2012- 2013 INTAKE 1. Th...

Published by Admin

MAKALA MBALIMBALI

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

Published by Admin

MICHEZO NA BURUDANI

Mshambulizi wa timu ta taifa ya soka ya Uganda Cranes, Uganda, Robert Ssentongo, ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano y...

Published by Admin

Mahakama yatengua ubunge wa Dr Kafumu :Igunga

By Mhariri - Aug 21, 2012

Link
MAHAKAMA KUU ya Kanda ya Tabora leo imemvua rasmi ubunge, Dk Peter Kafumu, aliyekuwa Mbunge wa Igunga kupitia Tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana. 

Hukumu hiyo imetolewa baada ya mlalamikaji Joseph Kashindye aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Tiketi ya Chadema kufungua kesi dhidi ya Peter Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo. Katika shauri hilo, hoja 15 ziliwasilishwa na wakili wa upande wa mlalamikaji Profesa Abdalla Safari ikiwamo anayodai kwamba Waziri wa Ujenzi John Magufuli alifanya mkutano wa kampeni Kata ya Igulubi wilayani Igunga kutumia madaraka yake kuahidi ujenzi wa Daraja la Mbutu kama wananchi hao watampigia kura mgombea wa chama mapinduzi.

Pia Safari anadai waziri huyo aliwatisha wananchi wa kata hiyo kwamba wasipo ichagua CCM daraja hilo halitajengwa na kwamba pia aliwatisha wananchi hao kuwa wasipomchagua Dk Kafumu watashughulikiwa.

Profesa Safari alidai Baraza la Waislamu (Bakwata) Wilaya ya Igunga liliwakataza waumini wasiipigie kura Chadema na kwamba naye Rais mstaafu, Benjamini Mkapa alitoa ahadi ya kugawa mahindi kwa wananchi wa Igunga siku moja kabla uchaguzi ili waichague CCM.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Pages 22123456 »