HABARI MPYA LEO  

Bob Diamond kuhojiwa na kamati ya Bunge

By Unknown - Jul 4, 2012

Bob Diamond

Aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa benki ya Barclays, moja ya benki kubwa zaidi nchini Uingereza, atahojiwa na kamati maalum ya bunge hii leo. Bwana Bob Diamond, ambaye alijiuzulu hiyo jana anatarajiwa kuhiojiwa kuhisana na sakata ya kuongezwa kwa viwango vya riba iliyopelekea kujiuzulu kwake.

Diamond, alijiuzulu hiyo jana baada ya benki ya Barclays kushutumiwa vikali kwa kuhujumu na kuongeza viwango vya riba kinyume cha sheria. Benki hiyo imepigwa faini mabilioni ya dola kufuatia kashfa hiyo.

Waandishi wa habari wanasema, Bwana Diamond atahojiwa kuhusiana na mazungumzo aliyofanya na naibu gavana wa benki kuu, wakati viwango hivyo vya riba viliongezwa.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII