Mzee Majuto kustaafu maigizo.
By Maganga Media - Jun 14, 2012
Mzee Majuto( Kushoto) akiwa na Sharo milionea
Nguli wa sanaa ya vichekesho Bongo, Amri Majuto ‘Mzee Majuto’ amesema anakaribia kuachana na fani hiyo iliyomletea umaarufu na heshima kubwa kote nchini.
Katika mahojiano ya dakika 30 aliyofanya na mtandao huu akiwa wilayani Bagamoyo Mzee Majuto alisema kuwa anataka kufanya kazi zake mwenyewe sambamba na vijana wachache aliowachagua kuepuka dhuluma anayokutana nayo kutoka kwa wajanja wanaotajirika kupitia migogo yao huku wakitoa malipo kiduchu kwa wasanii.
“Binafsi nalipwa Laki tano mpaka sita kwa filamu moja ambayo nina uhakika mtengezaji anakwenda kuingiza zaidi ya milioni themanini, sasa kuna haja gani mimi kuendelea kufanya kazi hizo”, alihoji Mzee Majuto.
Akiendela zaidi mchekeshaji huyo mwenye heshima kipee kwa wapenzi wa filamu nchini alisem akuwa si kama anaacha kuigiza moja kwa moja lakini atahamia katika kufanya kazi zake binafi tofauti na hizi za watu ili aweze kunufaika na jasho lake .
Hivi ninavokwambia tayari nimeshanunua baadhi ya vifaa vya kazi na baadhi nategemea kuvipata ifikapo mwezi wa 9 mwaka huu , alisema Majuto na kuongeza kuwa hakika nitageukia kwenye kufanya kazi zangu mwenyewe ili na mimi nifaidi jasho langu” alimaliza mchekeshaji huyo.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII