HABARI MPYA LEO  

Jamhuri Yawasilisha Ushahidi Wa Umri Wa Lulu.

By Unknown - Jun 23, 2012



MAWAKILI upande wa Serikali kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii nyota Steven Kanumba (28),inayomkabili msanii wa filamu Elizabeth Michael 'Lulu' wamewasilisha katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam vielelezo vya kuthibitisha kwamba mshtakiwa huyo ana umri wa miaka 18.

Vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani ni pamoja na CD iliyorekodi mahojiano kati ya Mtangazji, Maelezo ya kuomba hati ya kusafiria, na leseni ya udereva. Pia umewasilisha Mahakamani hapo maelezo ya Polisi pamoja na maombi ya hati kusafiria ambapo mshtakiwa ameeleza kwamba ana umri zaidi ya miaka 18.

Keshi hiyo itasikilizwa Juni 25 mwaka huu mbele ya jaji Dk.Fauz Twaib Mahakamani hapo.

Juni 18 Mawakili wa nutetezi Peter Kibatala , Fugency Massawe na Kennedy Fungamtama waliwasilisha vielelezo kwa njia ya maandishi kupitia kiapo.Katika ushahidi uliowasilishwa na baba mzazi wa Elizabeth Michael Kimeleta ameapa kwamba binti yake hadi anatuhumiwa kufanya mauaji , umri wake ni miaka 17.

Kalugira mama Mzazi wa Lulu anadai kuwa alimzaa mtoto huyo miaka 17 iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Jijini Dar es Salaam.

Upande wa Jamhuri unaoongozwa na Wakili nwa Serikali Shadrack Kimaro .Lulu anakabiliwa na shtaka la mauaji dhidi ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu , katika eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Juni 11, 2012 Mahakama Kuu ilikubali yenyewe kufanya uchunguzi huo kwa lengo la kubaini usahihi wa umri wa mshtakiwa huyo na ikaziagiza na kuzipangia tarehe pande zote katika kesi hiyo kuwasilisha mahakamani hapo vielelezo watakavyovitumia katika hoja zao.

Jopo la mawakili wanaomtetea Lulu likiongozwa na Kennedy Fungamtama Juni 13 waliwasilisha mahakamani hati za viapo vya wazazi wake na vielelezo vingine kikiwemo cheti cha kuzaliwa na cha ubatizo vinavyoonesha kuwa bado ni mtoto.

Lakini taarifa zilizopatikana mahakamani hapo zinaeleza kuwa vielelezo vilivyowasilishwa na Jamhuri vinaonesha kuwa mshtakiwa huyo ni mtu mzima kwa kuwa kwa mujibu wa vielezo hivyo ana umri zaidi ya miaka 18.

Viapo vya wazazi wa mshtakiwa huyo vilivyowasilishwa mahakamani hapo na Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Peter Kibatala ambaye ni mmoja wa mawakili wanaomtetea Lulu vinaeleza kuwa mshtakiwa huyo ana umri wa miaka 17. Viapo hivyo ni kiapo cha mama yake Lulu Lucresia Augustin Kalugila, mkazi wa Dar eS Salaam na kiapo cha baba mzazi Michael Kimemeta, mkazi wa Moshi.

Viapo vyote vinaeleza kuwa mshtakiwa huyo alizaliwa April 16, 1995 katika kituo cha Afya Muhimbili na kupewa cheti cha kuzaliwa namba B.0318479 cha Julai 23, 2004. Pia viapo hivyo vinaeleza kuwa baada ya kuzaliwa mshtakiwa, mama yake alimpa jina la Diana Michael Kimemeta, lakini alimpeleka mtoto huyo Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ndugu zake, walimpa jina la Elizabeth, jina la bibi yake Elizabeth Shikana.

Viapo hivyo vinaendelea kueleza kuwa baada ya majadiliano wote, yeye mama, baba na ndugu wengine walikubaliana kuwa wamuite Diana Elizabeth Michael Kimemeta . “ Elizabeth Michael Kimemeta alibatizwa katika Kanisa la Katoliki Chang’ombe Septemba 28, 1997 na alichukua majina ya ubatizo Diana Elizabeth Michael Kimemeta;” inasomeka sehemu nyingine ya kiapo hicho cha mama wa mshtakiwa.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII