AMISONI wateka ngome kuu ya Al-Shabaab!
By Maganga Media - May 26, 2012
Wanajeshi wa Muungano wa Afrika nchini Somalia wameuteka mji mihumu karibu na jiji kuu Mogadishu baada ya wapiganaji wa Kiisilamu kuondoka eneo hilo. Mji wa Afgoye umekua ngome kuu ya kundi la Al-Shabaab ambapo wapiganaji hao wanatumia eneo hilo kuulenga mji wa Mogadishu.
Wadadisi wamesema kwa kundi la Al- Shabaab kupoteza mji huo ni pigo kubwa, japo wapiganaji hao wanaaminika kujificha katika maeneo ya vichaka na mashamba ya karibu. Afgoye ambayo huwa Kaskazini Magharibi mwa Mogadishu ni njia muhimu inayounganisha maeneo ya Kaskazini, Magharibi na Kusini mwa Somalia.
Mji huu umetumika na wapiganaji wa Al Shabaab kulenga jiji la Mogadishu licha ya kutimuliwa mji mkuu na majeshi ya Muungano wa Afrika.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII