Stars msiwaogope kina DROGBA
By Maganga Media - May 31, 2012
NAibu waziri wa habari, vijana, Utamaduni na Michezo Amos makalla akimkabidhi bendera ya Taifa Nahodha wa Stars Juma Kaseja, wakati wa hafka ya kuiaga timu hiyo leo kwenye hoteli ya Tansoma.Stars inaondoka alfajir ya kesho kwenda Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wao wa mchujo wa komve la Dunia utakaopigwa juni mbil.Wengine ni meneja wa bia ya Kilimanjaro inayoidhamini9 timu hiyo George Kavise, Mwenyekiti wa BMT Dioniz Malinzi na Kocha wa Stars, Kim Poulsen.
KOCHA mkuu wa timu ya Taifa Taifa Stars amewataka wachezaji wake kutohofia nyota waliopo katika kikosi cha Ivory Coast kwani hawana tofouti na wao. Stars na Ivory Coast watachuana Juni 2, mjini Abidjan, katika mechi ya kuwania kucheza fainali za kombe la dunia ambapo kikosi cha Ivory Coast kinawachezaji wanaosakata soka la kulipwa barani Ulaya wakiwemo Didier Drogba, . Yaya Toure na Solomon Kalou na wengineo.
Kim alisema wanaiheshimu Ivory Coast kama moja ya timu yenye wachezaji wazuri lakini hawaihofii kwani wachezaji wa Stars pia ni wazuri ingawa wanatofaitiana vitu vidogo vidogo tu.
Kocha huyo aliwataka wachezaji wake kupambana kadiri wawezavyo katika mchezo huo kwani ndio siri ya ushindi na mafanikio ya timu yoyote.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII