Mnyika: Huu ni ushindi wa wananchi wa Ubungo!
By Maganga Media - May 25, 2012
Mara baada ya Mahakama kuu kutupilia mbali malalamiko mbalimbali ya kupinga ubunge wa mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika wa CHADEMA alisema kuwa ushindi huo ni wa wananchi wote. Akinukuliwa na mwandishi wa habari hii, Bwana Mnyika aliweka wazi kuwa kusema ni ushindi wake mnakosea kwani yeye alipigiwa kura na wananchi wa Ubungo, kura yake ilikuwa moja tu.
Kesi hiyo namba 107 ya 2010, ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Hawa Ngh’umbi dhidi ya Mnyika ambaye ni mdaiwa wa pili katika kesi hiyo akitetewa na Wakili Edson Mbogoro.
Mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo iliyoko mbele ya Jaji Upendo Msuya ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi (RO) katika jimbo hilo, (aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni) ambao walikuwa wakitetewa na Wakili Mkuu wa Serikali (PSA), Justice Mulokozi.
Katika uchaguzi huo, uliofanyika Oktoba 31, 2010, Msimamizi wa Uchaguzi, Raphael Ndunguru alimtangaza Mnyika kuwa mshindi Novemba 2, 2010 baada ya kupata kura 66,742. Ngh’umbi alipata kura 50,544.
Hata hivyo, Ngh'umbi hakuridhishwa na matokeo hayo akaamua kufungua kesi Mahakama Kuu kuyapinga, akimtumia Wakili Issa Maige.
Katika hati yake ya madai na wakati akitoa ushahidi mahakamani, Ngh’umbi na mashahidi wake walidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu na kisheria katika ujumlishaji wa kura na utangazaji wa matokeo ambao umeathiri matokeo hayo.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII