HABARI MPYA LEO  

Kesi ya BoT kusomwa Juni 25

By Maganga Media - May 24, 2012

 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Juni 25, mwaka huu itamsomea maelezo ya awali ya Kada wa CCM,  Rajabu Maranda  na wenzake watano akiwamo Ajay Somani na ndugu yake Jai Somani  wote wanakabiliwa na kesi ya wizi wa Sh 5.9 bilioni za Benki Kuu ya Tanzania (BoT).   Maranda na binamu yake Falijala Hussein wanatumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa Sh 1.8 bilioni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). 

Licha kusubiri kusomewa maelezo hayo ya awali, Maranda na Farijala  Juni 26, mwaka huu wanatarajiwa kusomewa hukumu nyingine kwenye kesi ya wizi wa Sh 2.2 bilioni  za  EPA za BoT.Wakili wa Serikali, Alapha Msafiri jana, alidai mbele ya Hakimu Ritha Tarimo kuwa, kesi ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Hakimu Tarimo alisema anaiahirisha hadi Juni 25, mwaka huu kwa sababu hakimu anayeisikiliza Hakimu Mfawidhi, Alvin Mgeta hayupo.

Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Maranda,  Farijala Hussein, Ajay Somani na ndugu yake Jai Somani pamoja na  wafanyakazi wawili wa BoT, Ester Komu ambaye anadaiwa kuwa wakati wizi huo unafanyika alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa  Idara ya Madeni na Bosco Kimela ambaye alikuwa Kaimu Katibu wa BoT.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII