Hollande atazindua sera mpya Ufaransa
By Maganga Media - May 7, 2012

Mgombea huyo wa chama cha kisoshalisti alipata 52% ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi huo.
Nicolas Sarkozy ndiye rais wa kwanza aliyekosa kuchaguliwa kwa awamu ya pili nchini Ufaransa tangu mwaka wa 1981. Rais Sarkozy anatarajiwa kumkabidhi madaraka Bw Hollande May 15.
Bw Hollande atakuwa rais wa kwanza wa kisoshalisti nchini Ufaransa, kwa kipindi cha miaka 17.
Punde baada ya kura za awali kuonesha matokeo, Rais Sarkozy alikiri kuwa ameshindwa, na alimpigia simu Bw Hollande kumtakia heri.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII