Chelsea wapokelewa kishujaa London
By Maganga Media - May 21, 2012
Baada ya ushindi wa kombe la UEFA huko Munich Ujerumani, Chelsea wamewasili London na kupokelewa na maelfu ya mashabiki.

.
Maelfu kwa maelfu ya mashabiki wanaimba na kushangilia kikosi cha Chelsea kilichoshinda Ligi ya mabingwa baada ya kurejea kutoka Munich kupitia mitaa ya London ya magharibi. Timu ya Chelsea ikisafiri juu ya mabasi mawili yaliyo wazi, ilianza msafara wake kutoka uwanja wa Stamford Bridge majira ya adhuhuri hapa London. Chelsea au maarufu kama The Blues' ilifanikiwa kushinda kombe la Ligi ya mabingwa kwa kuibwaga klabu iliyo shinda kombe le mshindi mara nne, Bayern Munich huko Ujerumani.

Ushindi wa kwanza. Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya London kushinda kombe la Ulaya.

Stamford bridge
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
