HABARI MPYA LEO  

Big Brother kuanza kesho

By Maganga Media - May 5, 2012


MSIMU mpya wa shindano la Big Brother umeanza kutimua vumbi na shindano hilo litang'oa nanga rasmi kesho, baada ya lile la mwaka jana lililomalizika Julai Mosi na Karen na Wendal kuondoka na mamilioni ya pesa.

Mkurugenzi wa M-Net, Biola Alabi amesema kama ilivyo kawaida ya shindano hilo ambalo huboreshwa kila mwaka, safari hii limeongezwa ubora mara dufu.

Amesema kuwa timu imejiandaa kuwaburudisha waafrika ambao ndio walengwa wakuu wa shindano hilo ambalo limekuwa likifanyika kwa miaka tano mfululizo. Shindano hili linafanyika kwa mara ya saba mwaka huu na Tanzania ikiwa mshiriki kwa miaka sita mfululizo.

Ndilo shindano pekee barani Afrika linaloonekana 'Live' saa 24 ndani ya miezi mitatu na kutazamwa na watu katika nchi 47. Wanzania waliowahi kushiriki katika shindano hilo ni  Mwisho Mwampamba, Richard, Latoya, Elizabeth,Bhoke na Lotus.

Zawadi inayoshindaniwa mwaka huu ni dola za Marekani laki tatu ambayo ni wastani wa shilingi za Tanzania milioni 480. Ingawa safari hii wanaingia washiriki wawili wawili lakini tunaambiwa ni mshiriki mmoja tu ndiye atakayeibuka mshindi.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII