TANGAZO LA AJIRA JESHI LA POLISI
By Maganga Media - Apr 4, 2012
Jeshi la Polisi liko katika mchakato wa kuajiri vijana kujiunga na Jeshi kupitia mashuleni.
Tumeamua kuurudia utaratibu ambao ulikuwepo zamani wa kuajiri moja kwa moja toka mashuleni ambao ulikuwepo siku za nyuma kutokana na mahitaji halisi ya Jeshi la Polisi kwa sasa.
Hivi sasa Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ongezeko la uhalifu mpya kama vile wizi wa kutumia mtandao, usafirishaji haramu wa binadamu na kadhalika. Wahalifu wanaohusika na matukio kama hayo, wamekuwa wakitumia mbinu mpya na utaalamu wa hali ya juu.
Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na Programu yake ya maboresho. Maboresho haya yanalenga kulifanya Jeshi kuwa la Kisasa zaidi ambalo litatelekeza majukumu yake kwa Weledi huku likiwa karibu zaidi na raia katika utendaji wake wa kila siku. Kutokana na changamoto hizo, Jeshi la Polisi linahitaji kuajiri, vijana wasomi, wenye utashi, ari na nia ya kufanya kazi za Polisi na wenye fikra na mtazamo unaoendana na dunia ya sasa.
Vijana hawa watakuwa viongozi na chachu katika kuleta mabadiliko yanayokusudiwa ndani ya Jeshi la Polisi.
A: – SIFA/VIGEZO VYA MWOMBAJI
- Mwombaji awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
- Awe na afya njema iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
- Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
- Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
- Awe amemaliza Kidato cha sita mwaka 2012 na kufaulu.
- Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.
B: MASHARTI KWA MWOMBAJI
- Kila mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Kila mwombaji awe na ari,utashi na nia ya kufanya kazi ya Polisi.
- Kila mwombaji aandike namba yake ya simu na anuani yake ya kudumu kwa usahihi ambayo itatumika wakati wa kuitwa kwenye usaili.
C: FOMU ZA KUJIUNGA ZINAPATIKANA:
- Ofisi ya Mkuu wa shule
- Ofisi za Makamanda wa Polisi Mikoa/Wilaya zilizo karibu
- Pata fomu hapa(sel-form)
Imetolewa na;
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P 9141,
DAR ES SALAAM.
FOR MORE DETAILS (CLICK HERE)
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII