ROSE MUHANDO aahidi kufunika tamasha la Pasaka
By Maganga Media - Apr 4, 2012
Rose Muhando |
MWIMBAJI mashuhuli wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki huo watakaojitokeza kushuhudia tamasha la Pasaka litakalorindima Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumapili.
Rose amesema atatumia fursa hiyo kutambulisha nyimbo zake saba zilizomo katika albamu yake ya Utamu wa Yesu ambazo ni Utamu wa Yesu uliobeba jina la albamu hiyo, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia. Rose alisema katika tamasha hilo atapata wasaa wa kuimba kwa
kushirikiana na mwanamuziki wa Kenya, Anastazia Mukabwa, aliyeimba kwa kumshirikisha
kwenye katika wimbo wa Vua Kiatu.
Tamasha hilo litasindikizwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa injili wakiwamo Rebecca Malope wa Afrika Kusini, Solomon Mukubwa, Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava, Faraja Ntaboba, Ephraim Sekeleti, Maryanne Tutuma, kundi la Glorious Celebration na kwaya ya Kinondoni Revival.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII