HABARI MPYA LEO  

ANGOLA YASHEREKEA MUONGO WA AMANI

By Maganga Media - Apr 5, 2012

Kulingana na takwimu za Benki Kuu ya Dunia, uchumi wa taifa hilo la Kusini mwa Afrika lenye watu zaidi ya milioni 20, umeongezeka kwa asilimia 12, likishika namba ya pili barani humo kwa usafirishaji wa mafuta baada ya Nigeria. Hayo yakitazamwa kama mafanikio makubwa kwa taifa la Angola, kukiwa na mafanikio ya ujenzi wa miundo mbinu kama vile barabara, viwanja vya ndege na mikakati ya ujenzi wa makazi mapya kwa baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. 

Lakini kwa upande mwingine, malalamiko yapo kwa utawala wa Rais Jose Eduard dos Santos kuwa amejilimbikizia mamlaka na kuwafanya wananchi wengi kuendelea kuwa masikini mno. Vijana wengi wanasadikiwa kukosa ajira, jambo ambalo limewafanya mara kadhaa kuingia barabarani kuandamana dhidi ya utawala. Vijana hao wakianza kufanya harakati kama zile za mataifa ya Kiarabu kuanza kufanya maandamano na kusisitiza kudai haki zaidi kutoka kwa utawala huo wa Angola pakiwa na miito mingi ya kufanya hivyo kwenye mitandao ya intaneti.

Marcolino Moco, ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa taifa hilo, ni miongoni mwa watu wanaoulalamikia utawala huu wa Rais Dos Santos akisema bayana kuwa sasa utawala wa Angola unatakiwa kutazama kwa kina hali ya siasa ulimwenguni ilivyo kama yale yanayotokea katika mataifa ya Kaskazini mwa Afrika huku uchaguzi wa Bunge ukipangwa kufanyika Septemba mwaka huu. Rais Dos Santos mwenye miaka 69 sasa, amekuwa kiongozi wa taifa hilo tangu mwaka1979.

CHANZO: DW

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII