HABARI MPYA LEO  

Syria kurudisha nyuma vikosi vyake

By Maganga Media - Apr 11, 2012

Maandamano nchini Syria
Moshi ulikuwa unachangiwa na mapambano baina ya Vikosi vya Serikali dhidi ya Wapinzani nchini Syria
REUTERS/Stringer

Moshi ulikuwa unachangiwa na mapambano baina ya Vikosi vya Serikali dhidi ya Wapinzani nchini SyriaSerikali ya Syria imeanza kuondoa Vikosi vyake katika maeneo ya makazi ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mapendekezo sita yaliyotolewa na Mpatanishi wa Kimataifa wa Mgogoro huo Kofi Annan ambayo yanatakiwa yametekelezwa hii leo kwa mujibu wa maafikiano yaliyowekwa.
Taarifa hizi zinakuja wakati huu Jumuiya ya Kimataifa ikiwa haina imani kama Syria inaweza kutekeleza hatua ya kuondoa Vikosi vyake katika Miji mbalimbali vikikabiliana na Wapinzani wanaoshinikiza mabadiliko ya utawala.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Walid Muallem amehakikisha kuanza kuondolewa kwa Vikosi hivyo na kurejea kwenye kambi za kijeshi lengo likiwa ni kupata utulivu katika nchi hiyo licha ya hapo jana kutaka kupata ufafanuzi Wapinzani wanapata wapi ufadhili.

Waziri Muallem ametoa hakikisho hilo wakati alipokutana na Waziri wa Mambo Nje wa Urusi Sergie Lavrov ambaye ametaka serikali ya Damascus kutekeleza pendekezo hilo la Annaa kwa vitendo kulingana na wakati uliopangwa.

Waziri huyo mwenye dhamana ya masuala ya Kimataifa wa Syria amesema kuwa vikosi sambamba na vifaru ambavyo vilikuwa kwenye Majimbo kadhaa nchini humo vimeondolewa ili kutekeleza maagizo yalitolewa na Mpatanishi wa Kimataifa Annan.

Kuanzia jana saa 11 alfajiri, umemalizika ule muda wa kuweka chini silaha nchini Syria, kwa mujibu wa mpango wa mjumbe maalum Kofi Annan. Idadi ya watu wanaokufa Syria inazidi kuongezeka licha ya kwamba siku ya kusitisha mapigano imefika. Katika muda wa saa 24 zilizopita watu zaidi ya 155 waliuawa ikiwa pamoja na askari 12 wa serikali. Mapigano makali zaidi yameripotiwa katika maeneo ya Homs, Aleppo na Daraa.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII