Libya yakataa kumpeleka Seif ICC
By Maganga Media - Apr 21, 2012
Serikali ya Libya, imeyaambia Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, kwamba ina ushahidi wa kutosha dhidi ya Saif Al Islam Gaddafi - mtoto wa kiume wa kiongozi wa zamani - kumfikisha mahakamani nchini Libya.
Mkuu wa mashtaka wa ICC, Luis Moreno Ocampo - ambaye anazuru Tripoli - alisema ameambiwa kuwa Libya itatoa hoja zake kwa ICC ufikapo mwisho wa mwezi huu. Saif Gaddafi anakabili mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu, lakini hadi sasa wakuu wa Libya wamekataa kumkabidhi kwa ICC.
Bwana Ocampo alisema ni jukumu la majaji wa ICC kutoa hukumu juu ya hoja za Libya.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII