HABARI MPYA LEO  

HOJA YA ZITTO YAKWAMA

By Maganga Media - Apr 21, 2012


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka Bungeni Mjini Dodoma,zinaeleza kuwa Kusudio la Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe la kutaka kupiga kura za kuanzishwa kwa mjadala wa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda,limepigwa chini na Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda.

Akisoma kanuni za Bunge,Mh. Spika alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge na Katiba ya Nchi,kusudio la kutaka kumuondoa Madarakani Waziri Mkuu kwa kupiga kura ya kutokuwa na Imani nae ambayo ni taarifa ya maandishi inapaswa kuwasilishwa kwake siku 14 kabla ya siku husika. Hivyo kwakuwa ofisi yake haijapata taarifa ya maandishi ju ya zoezi hilo,basi zoezi hilo moja kwa moja litakuwa ni batili, na kwasababu kikao hicho cha Bunge kinatarajiwa kufungwa siku ya jumatatu,basi hakutakuwa na uwezekano wa zoezi hilo kukamilika.

Awali Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamab aliomba muongozo wa Spika kuhusu jambo hilo ndipo Spika,Mh. Anne Makinda akasimama na kutoa ufafanuzi huo. Pia muda mfupi kabla ya kumalizika kikao Cha Bunge jioni ya leo mjini Dodoma,Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu alisimama kutaka muongozo wa Spika kuhusu Suala linaloendelea kwenye Bunge hilo la kukusanya Saini za wabunge wapatao 70 ili kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mh. Lissu alisema kuwa kitendo cha Spika kutoa uamuzi kwa jambo ambalo halijamfikia mezani kwake ni kama ukiukwaji wa kanuni na sheria za Bunge na itaonyesha kuwa kuna majibu yanaandaliwa kwa hoja ambayo hatakuiona bado hajaiona na kwa kufanya hivyo nikukiuka taratibu.

Baada ya Mh.Lissu kutaka muongozo huo,Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda alisema kuwa hajasema kwamba suala hilo si halali kufanyika ila alichosema halitawezekana kwa kikao hiki cha Bunge,kwa sababu linamalizika siku ya Jumatatu (23 April,2012), kwahiyo itakuwa ni vigumu sana kulifanya jambo hilo ndani ya Kikao cha Bunge hili.

Aidha akitoa ufafanuzi zaidi Mh. Spika mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Mh. John Mnyika,kusimama na yeye akitaka muongozo juu ya jambo hilo hilo ambapo alihoji kwamba,kuna tatizo gani kama watu wakiendelea kusaini (saini ambazo Mh. Mnyika alisema idadi yake imefikia 66 ) na kuwasilisha hoja siku ya jumatatu kwaajili ya kujadiliwa Bunge lijalo?

Mh. Anne Makinda alisema kwamba yeye hajasema kwamba jambo hilo halifai, "Naomba nieleweke na answered zitaletwa,sasa hivi nilicho kisema! nikwamba suala hilo haliwezekani kwa Bunge hili kwakuwa jumatatu ndio linafikia kikomo lakini kama mtaleta kwa kikao kijacho hakuna tatizo" alisema Makinda.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII