HABARI MPYA LEO  

Charles Taylor akutwa na hatia

By Maganga Media - Apr 26, 2012


Majaji katika mahakama maalum ya kimataifa wamempata na hatia Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor na hatia ya kufadhili vita nchini Sierra Leone. Katika kesi dhidi ya kiongozi huyo iliyochukua takribani miaka mitano alituhumiwa kwa kuwaunga mkono waasi ambao waliwaua maelfu ya raia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone kati ya mwaka 1991-2002.

Hata hivyo mahakama haijampata na hatia ya kuamrisha kutekelezwa kwa uhalifu wowote. Jaji mwandamizi wa kesi ya Charles Taylor Richard Lussick amesema mahakama inao ushahidi kwamba Taylor alifadhili kwa hali na mali maasi ya nchi jirani ya Sierra Leone.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII