Wanafunzi wanaosoma Kikorea (UDOM) wakiagana na mwalimu wao
By Maganga Media - Mar 22, 2012
Wanafunzi wa UDOM wanaosoma Kikorea wakiwa na Mwalimu wao, Cho Hye Chin (Wa tatu kutoka kulia waliokaa chini) Picha na Ronald Kessy |
Wanafunzi wanajifunza lugha ya Kikorea katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) leo wakiwa kwenye hafla fupi ya Kumuaga mwalimu wao aliyemaliza muda wake wa kuwepo nchini. Mwalimu Cho Hye Chin alifika chuoni hapa mwaka 2010 kufuatia mwanzilishi wa somo hilo hapo UDOM mwalimu Kim Son kumaliza muda wake. Walimu hao husambazwa na kampuni ya Wakorea ya KOICA yenye ofisi zake jijini Dar es Salaam.
Wakiongea katika hafla hiyo wamemshukuru sana mwalimu wao kwa ushirikiano aliowapa kwa kipindi chote akiwa chuoni hapo. Naye hakusita kuwatakia mafanikio mema katika masomo yao.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII