mazishi ya watoto waliouawa kwa kupigwa risasi Kusini mwa Ufaransa
By Maganga Media - Mar 22, 2012
Baadhi ya waombolezaji mjini Jerusalem nchini Israel |
Maelfu ya waombolezaji wamehudhuria mazishi ya watoto watatu na mwalimu wao yaliyofanyika viungani mwa mji wa Jerusalem nchini Israel, waliouawa baada ya kupigwa risasi katika shule ya kiyahudi mjini Toulouse Kusini mwa Ufaransa siku ya Jumatatu.
Miongoni mwa waombolezaji waliohudhuria katika mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe, pamoja na viongozi wengine wa serikali ya Isreal. Nchini Ufaransa Polisi wameendelea kumzingira mshukiwa wa tukio hilo katika makaazi yake mjini Toulouse na amekuwa akifanya mazungumzo na maafisa hao wa polisi kuhusu kujisalimisha kwake.
Polisi wanasema wanalenga kumkata mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 24 anayetambuliwa kwa jina la Mohammed Merah,ambaye amebainika pia kuwa raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria, akiwa hai ili afunguliwe mashtaka Mahakamani. Ndugu wa kiume wa mshukiwa huyo tayari amekamatwa pamoja na watu wengi wanaosadikiwa kuwa karibu naye na wanasaidia polisi kwa uchunguzi zaidi.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII