HABARI MPYA LEO  

WAASI WA MALI WAOMBA MSAADA

By Maganga Media - Mar 30, 2012

Kiongozi wa waasi waliopindua serikali, Amadou Sanogo ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia jeshi kupambana na waasi hao wa Tuareg ambao tayari wameuteka mji wa Kidal. Kiongozi huyo akisema kuwa jeshi linahitaji silaha za kupambana na waasi hao. 

Shirika la nchi za kanda ya Magharibi mwa Afrika, ECOWAS, limelaani kitendo cha wanajeshi, huku nchi hizo zikitishia kuiwekea vikwazo Mali. Viongozi wa nchi za magharibi mwa Afrika wamewapa wanajeshi waliopindua serikali ya Mali makataa ya saa 72 kuondoka madarakani au waadhibiwe kwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Mali kutoka kwa mataifa jirani ni moja kati ya hatua kali zinazochukuliwa kujaribu kuurejesha utawala wa Kidemokrasia uliopokonywa toka mikononi mwa Rais Amadou Touman Toure wa nchi hiyo wiki mbili zilizopita.

Jumuiya hiyo inatarajia kufunga mipaka yake yote ambayo hutumiwa na Mali katika shughuli za kiuchumi pamoja na kutimiza azma yake ya kuzifunga akaunti za nchi hiyo kama wanajeshi hao hawatatii amri ya kuachia madaraka jambo ambalo litadhoofisha kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi hiyo ambayo hupitisha mafuta yake katika nchi jirani ya Cote d`Ivoire.

Hii ni baada ujumbe mzito wa viongozi wa ECOWAS kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bamako kutokana na maandamano makubwa ya kuunga mkono mapinduzi hayo. Viongaoi wa ECOWAS,walikutana Ivory Coast, baada ya mpango wao kwenda kwa mazungumzo na viongozi wa wanajeshi waasi wa Mali kutibuka.

Hadi sasa Jumuiya na taasisi za kimataifa duniani tayari zimekwishaiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi. Umoja wa Ulaya na Marekani tayari zimesitisha utoaji wa fedha za miradi yote ya maendelo nchi humo na kubakisha misaada ya kiutu pekee. Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika pia zimo katika taaisisi za kimataifa zilizoiwekea vikwazo nchi hiyo.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII