HABARI MPYA LEO  

Afgnanistani; Marekani chukueni hatua!

By Maganga Media - Mar 22, 2012

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan Zalmai Rassoul

Serikali ya Afghanistan imeitaka Marekani kufanya uchunguzi halisi na wa wazi kuhusu jinai zinazofanywa na wanajeshi wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kitendo cha kuchoma moto kitabu kitakatifu cha Qur'ani na kuua raia wasiokuwa na hatia wa Afghanistan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan Zalmai Rassoul amewaambia waandishi habari mjini Kabul kwamba Waafghani wanasubiri kwa hamu kubwa kuona uchunguzi wa kuaminika ukifanywa na Marekani kuhusu kesi hizo mbili za askari wa nchi hiyo na kuwachukulia hatua wahusika. Amesisitiza kuwa uchunguzi kama huo wa kuamini ndio njia pekee ya kuboresha uhusiano ualioharibika wa Washington na Kabul.

Tarehe 20 Februari mwaka huu askari wa Marekani walioko kwenye kituo cha anga cha Bagram nchini Afghanistan walichoma moto nakala za kitabu kitukufu cha Qur'ani, suala ambalo limezusha machafuko makubwa ambapo raia wa Afghanistan na askari kadhaa wa Marekani wameuawa.

Machi 11 pia askari mmoja wa Marekani aliwamiminia risasi na kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya raia 16 wa Afghanistan wengi wao wakiwa watoto wadogo, na kujeruhi wengine wengi katika mkoa wa Kandahar.

Maganga Media

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII