Kizza Besigye akamatwa kwa kuongoza maandamano
By Maganga Media - Mar 22, 2012
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa na polisi baada ya kuongoza maandamano jijini Kampala siku ya Jumatano kulalamikia kupanda kwa bei za bidhaa, maandamano ambayo polisi inasema hayakuwa halali. Wakili wake,Ernest Kalibala hata hivyo anasema Besigye atafunguliwa mashtaka ya kuongoza maandamano yasiyo halali na ataachilia huru kwa dhamana.
Besigye alikamatwa pamoja na wanaharati wengine 16 huku polisi wakiwapiga wafuasi wa upinzani na kuwarushia gesi za kutoa machozi na kusambatarisha maandamano hayo. Polisi mmoja aliuawa katika purukushani hizo ambazo polisi wanasema mwenzao alipigwa jiwe kichwani akiwa katika harakati za kuwasambaratisha wafuasi hao.
Inaelezwa pia kuwa waandishi wa habari wawili walipigwa na polisi katika vurugu hizo siku ya Jumatano, suala ambalo muungano wa kutetea haki za waandishi habari umekashifu vikali. Besigye ambaye atafikishwa Mahakamani Ijumaa,amekuwa akikamatwa na polisi na kuachiliwa huru kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita kutokana na tuhma za kuongoza maandamano ya umma kulalamikia kupanda kwa bei ya bidhaa nchini humo.

Maganga Media
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII