HABARI MPYA LEO  

WATU Sita Wamepandishwa Kizimbani Mjini Singida, Kujibu Shitaka La Mauaji

By Unknown - Jul 17, 2012



VIJANA sita, Watuhumiwa wa mauaji ya Mwenyekiti UVCCM Yohana Mpinga wa Kata Ndago Iramba Singida, wakipandishwa kwenye gari la polisi

Afisa sera na utafiti CHADEMA Makao makuu, Waitara Mwita akifurahi na wanachama wa CHADEMA, baada ya kupata dhamana mjini Singinda
Mwita Waita (wa kwanza kushoto), akifurahi na wafuasi wa CHADEMA mahakamani mjini Singida, baada ya kupata dhamana ktk kesi ya mauaji.
Na: Elisante John.

Julai 16,2012.
WATU sita wamepandishwa kizimbani Mjini Singida, kujibu shitaka la mauaji ya Mwenyekiti UV-CCM Kata ya Ndago Wilaya Iramba,Yohana Mpinga, katika vurugu zilizohusisha wafuasi wa CHADEMA na CCM.
Wamesomewa shitaka hilo na mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Neema Mwanda mbele ya hakimu mfawidhi mahakama ya Mkoa Singida, RuthMassam.
Walioshitakiwa ni Manase Daudi (40), Williamu Elia (33), Frank Stanley (20), Charles Leonard (36), Tito Nintwa na Fillipo Edward (30), wakazi wa Ndago, Wilaya Iramba.
Wamedaiwa kufanya kosa hilo Julai 14, 2012 saa kumi alasiri, katika kijiji cha Nguvumali, kwa kutumia mawe na fimbo.
Hawakutakiwa kujibu lolote, kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kusikiliza kesi hiyo na itatajwa tena Julai 30, 2012.
Pia kesi nyingine iliyosomwa na mwanasheria wa Serikali Seif Ahmad, imemhusisha afisa sera na utafiti wa CHADEMA makao makuu Waitara Mwita (37) mkazi wa jijini Dar-es-salaam, akidaiwa kutoa lugha ya matusi mkutanoni.
Waitara anadaiwa kutoa lugha hiyo ya matusi dhidi ya Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, Julai 14, 2012 saa kumi jioni katika kijiji cha Ndago, Wilaya Iramba Mkoani Singida.
Yupo nje kwa dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja mwenye Sh.800,000 na itatajwa tena Julai 30, 2012.

NA MJENGWABLOG.COM

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII