HABARI MPYA LEO  

Polisi kuajiri 3000

By Unknown - Jul 19, 2012

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akiwasilisa bungeni makadirio na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/2013, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

JESHI la Polisi litaajiri askari wapya 3,000 wengi wao wakiwa wasomi kutoka taasisi za elimu ya juu.
Akiwasilisha makadirio ya Bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/13 katika kikao cha Bunge, Dodoma jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alisema:

“Sehemu ya waajiriwa itapatikana kutoka katika shule na vyuo vya elimu ya juu na idadi nyingine kutoka vijana wa JKT (Jeshi la Kujenga Taifa). Utaratibu huu unalenga kuwa na askari wenye sifa stahiki na waaminifu kwa kazi ya Polisi.”

Alisema polisi wataendelea kuongeza ufanisi katika upelelezi wa makosa ya jinai na kwamba mwaka 2012/2013 litatumia vyuo vyake vya Dar es Salaam na Kidatu kutoa mafunzo kwa askari wa kufanya kazi hiyo.

Dk Nchimbi alisema mafunzo hayo ya ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa za kiintelijensia na mbinu za kisasa za upelelezi, zitatolewa kwa maofisa, wakaguzi na askari wapatao 1,000.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII