HABARI MPYA LEO  

Okwi aibeba Uganda!

By Maganga Media - Jun 5, 2012

MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi ameibuka shujaa wa Uganda Cranes baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Angola katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014 uliofanyika jijini Luanda.Wenyeji Angola walipata bao la kuongoza mapema katika dakika ya saba lililofungwa na Campos Braume Manuel Abel Djalma. 

Uganda ilipata nafasi za kusawazisha bao hilo, lakini washambuliaji wake Mike Serumaga na Martin Mutumba walishindwa kutumia nafasi hizo walizozipata.  Zikiwa zimebaki dakika tano mchezo kumalizika kikosi cha Bobby Williamsons kilionekana kupotea kabisa mchezo ndipo Okwi alipokea mpira na kupiga shuti lililojaa nyavuni katika dakika ya 88.

Bao hilo la Okwi siyo tu limeinusuru Uganda na kipigo, lakini limeipa Cranes pointi moja muhimu katika jiji la Luanda na kushika nafasi ya pili Kundi J nyuma ya Senegal watakayopambana nayo wiki ijayo.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII