HABARI MPYA LEO  

Italia haoooo nusu fainali!

By Emmanuel Maganga - Jun 25, 2012

England na Italia

Timu ya England ya soka imeondolewa katika mashindano ya Euro 2012, baada ya kufungwa na Italia usiku wa Jumapili katika robo fainali, kwa kufungwa magoli 4-2 ya penalti mjini Kiev, Ukraine, kufuatia muda wa kawaida na dakika 30 zaidi kumalizika kwa timu hizo mbili kutofungana.

Italia sasa itapambana na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali.

Alessandro Diamanti alifunga bao la kuamua mshindi katika mikwaju hiyo ya penalti, baada ya Ashley Young na Ashley Cole kukosa kufunga mabao kupitia mikwaju waliyopiga. Vijana wa meneja Roy Hodgson ilikuwa wazi walilemewa katika mchezo mzima, lakini ni hali ya imani na uvumilivu iliwafanya kuwa na matazamio ya kuishinda Italia.

Italia iliweza kugonga mwamba, na bao la Antonio Nocerino lilikataliwa baada ya mwamuzi kusema aliotea mpira.

Kadri mechi ilivyoendelea, ndivyo wachezaji wa England nao walionekana wachovu, na ikielekea walitazamia bahati zaidi kuliko kujitahidi kuimarisha kiwango cha mchezo wao, na penalti kwao bila shaka ikawa sio za kutegemewa tena.

Baada ya mechi, nahodha Steven Gerrard alisema: "Wachezaji walicheza kadri ya uwezo wao wote. Nilidhani tungelipata bahati katika mikwaju ya penalti, lakini mambo hayakuwa hivyo. Ukiongoza katika penalti, unashikilia matumaini kwamba mambo yatasalia hivyo, lakini Italia ndio waliokuwa na bahati. Vijana waliokuwa walinzi walifanya kazi nzuri mno, na kuiletea nchi fahari, lakini tunarudi nyumbani na mioyo ya huzuni, na hili ni jambo gumu kulikubali."

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII