Taylor jela miaka 50
By Maganga Media - May 31, 2012
Upande wa mashtaka ulitaka kiongozi huyo wa zamani kusukumwa jela miaka 80. Charles Taylor amesisitiza hana hatia yeyote na anatarajiwa kukata rufaa. Akitoa hukumu hiyo Jaji Richard Lussick amesema dhuluma zilizotekelezwa nchini Siera Leone zilikuwa za kinyama zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya binadamu. Mahakama maalum ya Kimataifa inayochunguza dhuluma za kivita nchini Sierra Leone ilimpata Taylor na hatia ya makosa 11 dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.
Taylor amekuwa Rais wa kwanza kuhukumiwa kwa makosa ya vita na Mahakama ya Kimataifa tangu kesi za Nuremurgs dhidi ya watawala wa Kinazi baada ya Vita Kuu ya Pili duniani. Kesi dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Liberia inasikilizwa The Hague kwa hofu kwamba kufanyika kwake Sierra Leone huenda kukazua vurugu katika kanda hiyo. Taylor anatarajiwa kuhudimia kifungo chake nchini Uingereza.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII