HABARI MPYA LEO  

YANGA YAVULIWA UBINGWA RASMI

By Maganga Media - Apr 19, 2012

Kocha wa Yanga,Kostan Papic


MABINGWA wa soka nchini Yanga, wamechomoka ramsi kwenye mbio za ubingwa Ligi Kuu Bara na kuicha fursa hiyo kuwaniwa na mahasimu wao wakubwa Simba na Azam FC baada ya jana kupata kipigo wasichotarajia cha bao 1-0 toka Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mahasimu wao Simba walijiimarisha kileleni mwa msimamo baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu, matokeo yanayowafikisha pointi 56 ambazo kimsingi haziwezi kufikiwa na Yanga hata kama itashinda mechi zake tatu zilizosalia.

Yanga inabaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 43, na hata kama itashinda michezo yake mitatu iliyobaki, itafikisha pointi 52 ambazo zimeshapitwa na Simba, huku Azam yenye pointi 50 ikihitaji ushindi kwenye mchezo mmoja tu kuzipita pointi hizo za Yanga.

Lakini hata kama watakata rufaa na kurejeshewa pointi walizopokwa na Kamati ya Usuluhishi na Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), bado Yanga watafikisha pointi 55 ambazo tayari zimeshapitwa na Simba.

Katika mechi hiyo iliyojaa kila aina ya ushindani, shujaa wa Kagera Sugar aliyeipoteza Yanga kwenye ramani ya mbio za ubingwa alikuwa Shija Mkina aliyefunga bao pekee dakika ya 26.

Shija alifunga bao hilo akitumia makosa ya kipa wa Yanga, Yaw Berko aliyeshindwa kulinasa vizuri mikononi mwake shuti la adhabu ndogo lililopigwa na Mike Katende na mpira kumponyoka kabla ya kumkuta mfungaji.
 

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII