HABARI MPYA LEO  

Simba yatangaza Ubingwa

By Maganga Media - Apr 23, 2012

Klabu ya soka ya Simba imeukaribia ubingwa wa soka wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuichapa Moro United kwa magoli 3 kwa 0 katika mchezo uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba wametangaza kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwafunga Moro United na Azam kuwa wameng'ang'aniwa kwa sare dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Chamazi jijini Dar es Salaam. Mechi ya Azam na Mtibwa Suger imemalizika kwa sare ya moja kwa moja.

Vinara hao iliwachukua dakika 10 kupata bao kwanza lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na  Mafisango,  Haruna Moshi kupachika bao la pili dakika 33 na Felix Sunzu alifunga kalamu dakika 74.

Ushindi huo unaiweka Simba kwenye mazingira mazuri kabla ya mechi yake ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Alhy Shendi.

Chamazi, Mwamuzi Rashid Msangi alilazimika kumaliza mchezo dakika ya 88, baada ya wachezaji  Mtibwa Sugar kugomea penalti katika mchezo ulioshuhudia ubabe mwingi.

Dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho mwamuzi Msangi alilazimika kumaliza pambano baada ya wachezaji wa Mtibwa Sugar kutoka uwanjani wakigomea penalti.

Beki wa Mtibwa Juma Abuu aliunawa mpira kwenye eneo la hatari wakati akijaribu kuokoa na mwamuzi kuamua adhabu hiyo, ndipo wachezaji wa Mtibwa walipomzonga kupiga uamuzi huo.

Vinara hao walitawala zaidi sehemu ya kiungo na kufanya mashambulizi mengi langoni kwa Moro United iliyoingia uwanjani ikiwa na wachezaji wanne wanaolipwa mshahara na Simba waliowachukua kwa mkopo ni beki Meshack Abel, Salum Kanoni, Godfrey Wambura na Kelvin Charles.

Kiungo Haruna Moshi alifunga bao la pili kwa Simba katika dakika ya 33 akiunganisha vizuri krosi ya Uhuru Seleman.

Mshambuliaji Emmanuel Okwi alipoteza nafasi nzuri ya kuifungia Simba bao la tatu kwa kushindwa kumalizia kwa umakini krosi ya Uhuru katika dakika ya 36.

Moro walijibu mapigo dakika moja kabla ya mapumziko kwa shuti la beki Erick Mawala kugonga mwamba wa juu, lakini kipa Juma Kaseja alikuwa makini na kuwahi kudaka.


Ushindi kwa vinara Simba umewafanya wafikishe pointi 59 na kubakiwa na mechi moja dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga, wakati sare kwa Azam imewafanya wawe na pointi 51 huku wakibakisha mechi mbili baada ya leo. Azam inaendelea na harakati za kusaka nafasi ya pili. 

Kwa matokeo hayo, ‘Wanamsimbazi’ watatwaa ubingwa na kuwapoka taji hilo mabingwa watetezi, mahasimu wao wa jadi, Yanga.

SIMBA WAMNASA NIZAR KHALFAN

KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan aliyekuwa anacheza soka ya kulipwa Marekani, amejiunga rasmi na `Mabingwa Watarajiwa’ wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu, Simba.
Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa, usajili wa mchezaji huyo umefanikishwa na mmoja wa wafadhili wa zamani wa klabu hiyo, Azim Dewji.


YANGA YAAHIDI KULINDA HESHIMA


BAADA ya kupoteza harakati za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Yanga imejinasibu kushinda michezo yake iliyosalia kwenye ligi hiyo ili kulinda heshima.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII