SAJUKI AZUNGUMZIA AFYA YAKE
By Maganga Media - Apr 24, 2012
Sajuki kabla ya kuumwa. |
Baada ya stori kuenea kwamba Mwigizaji Juma Kilowoko maarufu kama SAJUKI amefariki dunia, amejitokeza mwenyewe na kuzungumzia hizo stori.
Sajuki amesema “mimi ni Sajuki ninaezungumza, unajua nikwambie siri moja, nilikaa nilifikiria, kwanza nilishituka sana mwenyewe japokua naona kama wananiongezea uhai, wanaiombea dua ya uhai”
Katika sentensi nyingine Sajuki amesema “unajua majuzi kati mke wangu Wastara alikua anawaambia watu juu ya kuumwa kwangu na namna gani tunavyohitaji watu watusaidie sasa pengine maadui wakaona kwamba watanzania wameshituka sana wameona watatusaidia, wenyewe ndio wakaamua kuchafua chafua vitu kama hivyo kwa hiyo ni habari za kizushi, mimi niko fesh tu hapa sasa hivi”
Amesema “niko kwenye mpango wa kufanya movie yangu mpya ambayo nitaisimamia, hata hizo habari zilipoanza kutoka nilikua kwenye maandalizi ya movie yangu nikashtuka nikasema heee nimekufa niko location jamani hata watu niliokua nao wakawa wanashangaa, wakati ukifika utafika mwenyenzi Mungu akiamua kunichukua atanichukua, sawa mimi naumwa lakini sio kwenye hiyo hali ambayo watu wanaielezea, pamoja na kuumwa kwangu sasa hivi nipo kama Rambo napigana bado.
SOURCE: millardayo.com
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII