KAULI YA WAZIRI MKUU
By Maganga Media - Apr 21, 2012
Waziri mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda amesema kuwa hajapokea barua yoyote ya Waziri kujiuzuru na kama kutakuwa na taarifa zozote atazungumza siku ya Jumatatu wakati wa kuhitimisha shughuli za Bunge |
Baada ya kuwepo kwa taarifa za mawaziri nane kujiuzulu, leo baada ya spika wa bunge ANNA MAKINDA kuahirisha kikao cha bunge mpaka siku ya jumatatu. Waziri mkuu MIZENGO PINDA amesema”sijapokea barua yeyote kutoka kwa waziri yeyote kujiuzulu kama wapo watatuletea ila kwa upande wangu sijapokea barua yeyote.
Pia kuhusiana na habari kuandwa kwenye magazeti sijafanikiwa kusoma na wala sina uhakika na kilicho andikwa . Ila kwa yeyote ambaye anayetaka kujua lolote kuhusu taarifa hizi ntatolea ufafanuzi siku ya Jumatatu”.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa awali juu ya tetesi hizo, zilidai kuwa chanzo cha taarifa hizo ni kutoka kwenye kikao cha wabunge wa CCM kilichoitishwa na waziri mkuu jana usiku baada ya kuahirisha shughuli za Bunge.
Nao wabunge mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walipohojiwa na vyanzo mbalimbali vya habari leo mchana hawakuwa tayari kuzungumza juu ya taarifa zozote za kikao cha jana hadi hapo taarifa zaidi kwa mujibu wa Waziri mkuu kama zitakuwepo zitatolewa siku ya Jumatatu atakapokuwa anahitimisha shughuli za Bunge.
Uongozi wa blogu ya Maganga Media unaahidi kuwa utajitahidi kuendelea kuandika habari na taarifa zingine muhimu kwa jamii kutoka katika vyanzo halisi ili kuepusha upotoshaji wa taarifa kwa Wananchi. Aidha tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza juu ya vyanzo mbalimbali vya habari juu ya tukio hili.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII