HABARI MPYA LEO  

Arsenal hoi kwa Wigan

By Maganga Media - Apr 17, 2012

Roberto Martinez kocha mkuu wa Wigan akifurahia ushindi wa timu yake
Roberto Martinez kocha mkuu wa Wigan akifurahia ushindi wa timu yake

Ligi kuu nchini Uingereza imeendelea siku ya jumatatu kwa kushuhudia mchezo mmoja pekee ukipigwa kwenye dimba la Emarates kati ya wenyeji Arsenal waliowakaribisha vijana wa Wigan Athletics.

Mchezo huo ambao ulikuwa muhimu kwa timu zote mbili, ambapo wakati Arsenal ilikuwa ikihitaji ushindi ili kuendelea kusalia kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, Wigan wenyewe walikuwa wakihitaji ushindi ili kujinasua kwenye wimbi la kutaka kushuka daraja.

Wigan waliokuwa wa kwanza kujiandikia bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji wake Franco Di Santo ambaye alipachika bao hilo katika dakika ya 7 ya mchezo. Kabla Arsenal hawajajipanga kurejesha bao, walijikuta wakiruhusu bao la pili kwenye dakika ya 8 ya mchezo bao ambalo lilifungwa na Jordi Gomez aliyetumia uzembe wa mlinda mlango wa Arsenal na kuiandikia bao la pili timu yake.

Arsenal walizidisha mashambulizi  kwenye kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 27 ya mchezo lililofungwa na Thomas Vermaelen aliyeunganisha mpira wa kichwa.

Kwa matokeo hayo Arsenal imeendelea kusalia kwenye nafasi yake ya nne kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 64, wakati Wigan wamechumpa hadi kwenye nafasi ya kumi na sita wakiwa na alama 34.

Msimamo wa ligi unawaonyesha Manchester United wakiongoza ligi wakiwa na alama 82 wakati Manchester City wakiwa na alama 77, huku mkiani mwa ligi hiyo kukiwa na timu ya Wolves, Blackburn na Bolton.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII