RAIS MPYA WA UJERUMANI AAPISHWA
By Maganga Media - Mar 23, 2012
Rais mpya wa Ujerumani, Joachim Gauck (Kulia) akiapa leo |
Siku 5 baada ya kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Ujerumani,Joachim Gauck ameapishwa rasmi mbele ya wabunge wa mabaraza yote mawili,bunge la shirikisho Bundetag na baraza la wawakilishi wa majimbo Bunderat mjini Berlin. Spika wa bunge la shirikisho Bwana Norbert Lammert alifungua hafla hiyo maalum .Spika wa bunge amesema kuchaguliwa Gauck ni ushahidi wa maendeleo katika kukuwa pamoja wakaazi wa mashariki na magharibi ya Ujerumani.
Spika wa baraza la wawakilishi wa majimbo Bundesrat Horst Seehoffer amesema kuchaguliwa Joachim Gauck ni hatua muhimu katika historia ya Ujerumani."Mwanatheolojia wa Mashariki alikuwa mstari wa mbele katika mapinduzi ya amani ya mwaka 1989 katika Ujerumani mashariki ya zamani,amesema mwenekiti huyo wa chama cha kihafidhina cha CSU aliyeidaka kauli mbiu ya wakati ule "Wananchi ni sisi".
Maganga Media
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII