HABARI MPYA LEO  

Papa aitaka jamii kuwalinda watoto

By Maganga Media - Mar 25, 2012

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani,Papa Benedict xvi
Akiwa ziarani nchini Mexico, Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Benedict wa 16 ametoa wito kwa jamii kuwajali na kuwalinda watoto sambamba na kutuma ujumbe maalumu kwa kundi lililoathirika baada ya ghasia. Huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia papa Benedict wa 16 alitaja kashfa ya matendo mabaya dhidi ya watoto inayomuhusisha kuhani wa katoliki katika kipindi cha hivi karibuni.

Hii ni ziara ya pili kwa kiongozi huyo kutembelea bara lenye idadi kubwa ya wakatoliki duniani akisisitiza kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya na vitendo viovu dhidi ya ubinadamu.
Katika ziara yake kiongozi huyo wa katoliki duniani anatarajia kujadili mambo mbalimbali na raisi Felipe Caldero ikiwemo masuala ya uhalifu uliokithiri pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Papa amesema yeye ni mgeni wa kuleta matumaini. Amesema anataka kuwasaidia Wamexico kubadilisha maisha yao, na amelaani ghasia zinazohusika na madawa ya kulevya, ambazo zimeuwa maelfu ya wananchi katika miaka ya karibuni.


Maganga Media

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII