UTII WA SHERIA BILA SHURUTI
By Unknown - Jul 17, 2012
RASIMU YA ANDIKO LA MPANGO WA KAMPENI YA UTII WA SHERIA ZA NCHI BILA SHURUTI
UTANGULIZI
Jeshi la Polisi Tanzania kwa kushirikiana na wadau wakewa HAKIJINAI, limeanzisha kampeni ya kuiwezesha jamii kutambua umuhimu wa utii wa sheria za nchi na taratibu za jamii bila shuruti.
Kampeni hii ni moja ya juhudi zinazolenga kuboresha maadili ya jamii kama msingi wa maendeleo yanayozingatia usalama, amani na utulivu ambazo ni nguzo za ustawi wa kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
Msingi wa kampeni hii unalenga kuongeza ari na moyo wa uzalendo unazingatia uwajibikaji katika harakati za kujiletea maendeleo bila kuvuja sheria za nchi.
LENGO KUU
Kuongeza kiwango cha utii wa sheria za nchi bila shuruti jambo ambalo litasaidia kupunguza uhalifu na matumizi ya shuruti katika usimamizi ya utiifu wa sheria za nchi. Utaratibu huu pia utasaidia kupunguza gharama katika oparesheni za kupambana na uhalifu.
Aidha, utii bila shuruti utasaidia kupunguza msongamano wa kesi mahakamani na idadi ya wafungwa/mahabusu wanaotakiwa kuhudumiwa na Idara mbalimbali kwa kodi za wananchi.
BAADHI YA FAIDA ZA KAMPENI YA UTII BILA SHURUTI
Kampeni hii ina faida nyingi, baadhi ya faida hizo ni:-
1. Kuiwezesha jamii kuishi salama kwa amani na utulivu kwa kutii sheria bila shuruti hivyo kuepusha migogoro na vurugu.
2. kupunguza hali ya watu kuishi kwa shaka au wasiwasi wa kudhurika na matendo ya kihalifu.
3. Kupunguza wananchi wanaokaidi kutii sheria za nchi na kupelekea matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima dhidi yao
4. Kuongezeka kwa ushirikiano baina ya vyombo vya dola na jamii
5. Kupunguza idadi ya migogoro ya kisheria, yaani washitakiwa au walalamikaji.
6. Kupunguza mrundikano wa kesi na kuboresha utendaji wa wadau wa HAKIJINAI.
7. kuwa na jamii adilifu, inayojali utiifu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi kwa maendeleo endelevu. unaolenga kuboresha maadili ya uwajibikaji na utii sheria za nchi na taratibu za jamii kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa.
WADAU MUHIMU
1. Jamii kwa ujumla
2. Vyombo vya dola, Wizara na taasisi ambazo ni wadau wa
HAKIJINAI.
3. Vyama vya siasa
4. Taasisi za kijamii (Vyombo vya habari, madhehebu ya dini,
asasi nk).
BAADHI YA HATUA MUHIMU ZA UTEKELEZA
Mpango huu wa kuhamasisha jamii kutii bila shuruti, utakuwa na mpango mkuu na mipango midogomidogo ambayo italenga kutimiza mpango mkuu katika kila himaya. Kila himaya, kuanzia makao makuu, Mikoa, wilaya hadi vituo wataweka utaratibu wa kuwezesha jamii kutambua na kuchukua hatua za kutii bila kungoja
kushurutishwa.
Aidha, kwa hatua ya awali mambo yafuatayo yatatekelezwa:-
1. Kuzindua mpango huu kitaifa
2. Kuwawezesha Makamanda wa Mikoa yote kutambua jinsi ya
kutekeleza mpango huu
3. Kuwawezesha taasisi ambazo ni wadau wa haki jinai kutambua
na kutumia fursa katika kutekeleza mpango huu.
4. Kudai mrejesho kila robo ya mwaka.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII