HABARI MPYA LEO  

Blatter alifahamu kuhusu rushwa

By Emmanuel Maganga - Jul 13, 2012

Rais wa sasa wa shirika linalotawala mpira duniani Fifa Bw.Sepp Blatter alifahamu kuwa wakuu wenzake wanapokea mlungula, kwa mujibu wa uchunguzi uliofichuliwa na Mahakama kuhusu ruishwa.

Aliyekuwa Rais wakati huo Joao Havelange pamoja na mwanachama mkuu wa kamati ya utendaji Ricardo Teixeira walitajwa jumatano katika tuhuma za kupokea mlungula kutoka kampuni inayoshirikiana na FIFA kama mkondo wake wa biashara na masoko.ISL.

Hakuna baina yao aliyelaumiwa na FIFA wala kuonywa.

Kwenye wavuti ya Fifa, Sepp Blatter anasema kuwa alifahamu kuhusu malipo hayo ingawa ameongezea kusema kuwa yalikua halali wakati ule.

Blatter amesema kuwa, wakati huo, malipo ya aina hiyo yangeweza hata kukatwa kutoka kwenye fungu la kodi kama gharama za biashara. Kwa leo, hilo linaonekana kuwa tendo la kihalifu.

Korti moja ya Uswizi iliamuru nyaraka zilizofichua kisa hicho na Maofisa waliohusika waliopokea mlungula kutoka kampuni ya ISL watajwe.

Kampuni hiyo ya ISL ilifilisika mnamo mwaka 2001.

Nyaraka zilizotaja majina ya Maofisa wa Fifa waliohusika ziliruhusiwa kuchapishwa na vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na BBC, zikitowa maelezo kamili yaliyohitimishwa mnamo mwezi Mayi mwaka 2010.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII