HABARI MPYA LEO  

Mganga kutoka UDOM!

By Unknown - Jun 26, 2012

Haya tena yule mtaalamu amewadia. Anakuja kutoa suruhu ya matatizo yako sugu! Kaa tayari. Ungana naye hapa chini anavyonadi biashara yake!

Kufuatia wito wa Raisi kwamba wahitimu tujiajiri hivyo naenda kujiajiri kwa kufungua kituo cha “Tution” huko urambo. Tangazo la kituo changu litakuwa kama ifutavyo:

Kwa wale wanafunzi wagonjwa wa Kiswahili wenye matatizo ya kushindwa kutunga na kuchanganua sentensi,kushindwa kujibu maswali ya vitabu, mwandiko mbaya, kushindwa kujibu maswali ya ufahamu, kushindwa kubainisha aina za maneno na mambo yote yanayohusu lugha ya Kiswahili, suluhisho limepatikana, ni mganga kutoka UDOM ndugu Marco Henry amekuja na dawa kali ya Shahada ya Awali ya Isimu ya Kiswahili kwa ajiri ya kutatua tatizo lako, wewe mwl wa grade A, mwl wa diploma, wanafunzi wa msingi, sekondari na vyuo kwa nini uendelee kuteseka kwa muda mrefu njoo uonane na mganga huyu na tatizo lako litaisha ndani ya siku chache kwa bei nafuu. Garantii ya dawa ni milele.

Mawasiliano, simu: 0782178350 / 0754821152/0716167026
Email; mhmapalala@gmail.com. Facebook; Marco Henry
BLOG: MAPALALA MEDIA

KARIBUNI SANA
· · · June 22 at 1:07am

HII INAPASWA KUINGIA KWENYE ORODHA YA TANGAZO KALI LA MWAKA! KILA LA KHERI WAHITIMU WA SHAHADA ZAO ZA KWANZA KATIKA FANI MBALIMBALI KUTOKA UDOM NA VYUO VINGINE NCHINI!

Maganga Media inawatakia mafanikio mema huko muendako. Tunaondoka kwenye maisha ya maigizo sasa tunaenda kwenye maisha halisi. Ni jukumu lako kubadilisha mtazamo wa maisha ili utoke kimaisha. To God be the Glory!

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII